loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC azuia ‘kishika uchumba’ mazao ya viungo

MKUU wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mwanaasha Tumbo amepiga marufuku vitendo vya wakulima wa mazao ya viungo kuyauza yakiwa bado hayajakomaa kwa kuwa wananyonywa na kuwanufaisha wafanyabiashara.

Alitoa agizo hilo jana wakati wa kikao cha Jukwaa la Mazao ya Viungo lililofanyika katika kata ya Nkumba.

Mwanaasha alisema mkulima atakayebainika anauza mazao hasa ya viungo kabla hayajakomaa atachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa atakuwa anahujumu jitihada za serikali za kumkomboa mkulima.

"Kuna tabia imezuka ya kutoa kishika uchumba katika mazao yakiwa shambani naomba niaambie hicho kishika uchumba kinalengo la kumnyonya mkulima mdogo kwani bei ya viungo vikiwa tayari kwa kuuza ni mara ya hicho mnachopewa mazao yakiwa machanga"alisema.

Mwanaasha aliwataka wakulima wazingatie taratibu walizojiwekea kuhakikisha wanauza mazao yaliyokomaa kwa bei elekezi katika vituo ambavyo vipo wilayani humo.

Alimuagiza Mwanasheria wa Halmashauri hiyo aandae Sheria Ndogo ya Kilimo na Uvunaji ili watakaoivunja wachukuliwe hatua.

Ofisa Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Wilaya Muheza Hoyange Marika aliwataka wadau wa kilimo na wakulima wajisajili katika daftari maalumu ili waweze kusaidiwa kwa haraka na serikali changamoto zinazohusu masuala ya kilimo  zinapojitokeza.

"Ili kufanya kilimo chenye tija sisi Halimashauri tumeandaa daftari maalum ambalo litakuwa na takwimu halisi za wakulima wa mazao yote hivyo itasaidia kushauriana na kutoa maelekezo kwa walengwa kwa wakati mwafaka"alisema Marika.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Amina Omari, Muheza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi