loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ruangwa wavuna bil 20/- mauzo madini

WILAYA ya Ruangwa mkoani Lindi hadi Novemba mwaka huu imepata jumla ya Sh 19,909,123,260.29 za mauzo ya madini ya dhahabu na magonga (Green garnet) tangu kuanzishwa kwa soko la madini wilayani humo Mei mwaka 2019.

Kaimu Ofisa Madini Mkazi Mkoa wa Lindi, Jeremiah Hango aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na HabariLEO ofisini kwake wilayani Nachingwea.

Alisema katika kipindi hicho kilogramu 165.53 za dhahabu ziliuzwa kwa Sh 19,679,862,873.84 na pia madini aina ya magongo (Green Garnet) yaliingiza Sh 229,260,386.45.

Hango alisema katika kipindi hicho serikali ilipata mapato ya kodi jumla ya Sh 1,453,204,389 ukiwemo mrabaha Sh 1,194,547.395.62, ada ya ukaguzi Sh 198,929,624.27, na tozo ya huduma Sh 59,727,369.78.

Alisema, kabla ya kufunguliwa soko hilo madini mengi yalikuwa yakitoroshwa hivyo lilianzishwa soko hilo kwa kushirikiana na vituo vya ununuzi vilivyoko katika mgodi wa Namungo wilayani Ruangwa na Kiegei katika Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi.

Aliwataka wamiliki wa migodi wenye leseni maeneo yao kuna mashamba ya wakazi walipe fidia kwa kufuata taratibu na sheria za mamlaka ilizoweka.

Hango alisema, mwenye leseni ML521/2014 na ML524/2014 zinalalamikiwa kwa kutolipa fidia ya mashamba na nyumba za wakazi walioko ndani ya eneo la leseni hizo kwa kuwa awali kulikuwa na mashamba ya wakazi wakilima katika mgodi wa Namungo, wilayani Ruangwa.

Katika kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka katika vivutio vya ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Nachingwea

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi