loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watafiti watakiwa kujikita kusambaza elimu ya walichofanya

WANAZUONI Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) wamepongezwa kwa kufanya tafiti mbalimbali zinazogusa maendeleo ya wananchi na  kushauriwa kutumia tafiti hizo kueleza namna bora ya kuunganisha vipaumbele vilivyopo tangu ngazi ya taifa hadi vijijini ili vishabihiane na azma ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Akizungumza katika Kongamano la 12 chuoni Hombolo lililoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Gerald Mweli, Mchambuzi wa mada tatu zilizowasilishwa kuhusu uongozi, Jumanne Sagini alisema wanazuoni hao wamefanya kazi nzuri ya utafiti huo sasa wajikite kutafuta suluhisho la namna bora ya kuunganisha vipaumbele vingi vilivyopo nchini ili viwe chachu ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Sagini ambaye ni Mbunge wa Butiama mkoani Mara alisema kuna vipaumbele vingi nchini vikiwemo vilivyopo kwenye Ilani ya Uchaguzi, vipo katika mikoa, katika wilaya, tarafa, kata, vijijini ambavyo kama vitatafutiwa namna bora ya kuunganishwa vitasaidia kuwapatia wananchi maendeleo.

“Kuunganisha kwa vipaumbele vya kitaifa vya kujenga miradi ya kimkakati, vya mikoa, vya wilaya , tarafa, kata hadi vijijini viunganishwe kwenye nchi ya uchumi wa kati ili uchumi huo uonekane unatoa mchango wa kuinua maisha ya wananchi,” alisema.

Alisema pamoja kuunganisha vipaumbele ili kuleta maendeleo kwa wananchi, wanazuoni hao wanao wajibu wa kufanya utafiti wa kuunganisha wataalamu, viongozi wachaguliwa na kuwaunganisha wananchi ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa maendeleo.

Kangamano hilo lililokuwa likiongozwa na Dk Peter Mateso, Sagini alisema wanatakiwa pia kuziangalia sera mbalimbali nchini zikiwemo za vyama vya upinzani nchini ambazo badala ya kuhimiza wananchi kuchangia nguzu zao katika kuleta maendeleo zinapinga, hivyo kuwanyima fursa wananchi kupata miradi ya maendeleo wakingoja serikali kufanya kila kitu.

Alisema watafiti hao wanaweza kutafuta suluhu kwani suala la kujitolea halipo Tanzania tu hata katika nchi zilizoendelea, hivyo ni wajibu wa watafiti kuja na suluhisho la kurudisha moyo wa watu wa kujitolea ambao umeshuka sana.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Mifugo, Sekta ya Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel alisema katika kufanikisha hayo, nguvu ya viongozi wateule au wanaochaguliwa katika kuhamasisha jamii kushirikisha katika kazi za kuleta maendeleo ni kama gundi katika kukuza maendeleo ya nchi.

Profesa Gabriel alisema viongozi hao wakitaka kuwavuta wanajamii kushiriki katika kujitolea, wanatakiwa waongoze kwa mifano na kushirikiana nao na kufanya kazi kama timu hata kushiriki katika mijadala mbalimbali na kuwasiliana nao kwa nyuso za kuvutia.

Naye Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), Dk Mpamilwa Madale alisema waliamua kuweka mada ya kuwakumbusha viongozi waliochaguliwa au kuteuliwa wajibu wao kutokana na wakati wenyewe kuwa mwafaka kwani ndio kwanza wametoka kuchaguliwa ili wajue wajibu wao wanatakiwa kutekeleza hasa wa kushirikisha jamii katika kuleta maendeleo.

Dk Madale alisema wanazuoni wamejipanga kuendelea kufanya utafiti mbalimbali ili kuibua changamoto za wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo pia litahamasisha viongozi hao kujituma na kushirikisha jamii katika kujenga miundombinu kwa ajili ya maendeleo yao.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi