loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba kuivaa Plateau Jumapili

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, Simba wamefanya mazoezi jana baada ya kufika salama Abuja, Nigeria kwa ajili ya mchezo dhidi ya wapinzani wao Plateau FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa New Jos katika mji wa Jos na kurudiana Dar es Salaam Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Kwa mujibu wa mratibu wa kikosi hicho, Abbas Ally alisema kikosi hicho kilifika salama na kwamba watapambana kupata ushindi na kurudi nyumbani mapema kujiandaa na mchezo wa marudiano.

“Mazingira ni mazuri tumepata ushirikiano mzuri kutoka kwa shirikisho la soka la hapa, hali ya usalama pia ni nzuri matumaini yetu ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo,” alisema.

Wachezaji 24 wa Simba wapo nchini humo kujiandaa na mchezo huo wa hatua ya awali wa kimataifa.

Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kupata ushindi ili kumaliza kazi mechi ya marudiano na kuvuka kwenda hatua nyingine.

Simba ambao msimu uliopita hawakufanya vizuri baada ya kutolewa hatua za awali na UD Songo ya Msumbiji wamedhamiria kurudi katika kiwango kizuri ili kuandika historia nyingine baada ya mwaka juzi kuingia nane bora ya michuano hiyo.

Iwapo Simba itafanikiwa kuiondoa Plateau itakutana na mshindi kati ya CD Do Sol na FC Platnum.

Mwakilishi mwingine katika michuano ya kimataifa ni Namungo anayetarajiwa kumkaribisha Al Rabita FC ya Sudan Kusini katika michuno ya Kombe la Shrikisho Afrika.

Namungo iliyopanda kucheza Ligi Kuu msimu uliopita itaweka historia kwa mara ya kwanza kuwakilisha nchi katika michuano hiyo.

TIMU ya soka ya Yanga Princess imezidi kujikita kileleni baada ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi