loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yaanza kurejea taratibu

WENYE ligi yao wameanza kurejea kwenye nafasi zao. Hivyo ndio tunaweza kusema baada ya Yanga kuifunga Azam FC 1-0 na kushika uongozi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuwaondoa vijana hao wa Bakhressa waliokalia nafasi hiyo kwa muda mrefu.

Mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, ambao ulijaa ushindani mkali kutokana na ubora wa vikosi vyote timu iliyopewa nafasi ya moja kwa moja kuibuka na ushindi.

Yanga kwenye mchezo huo waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kufikisha pointi 28 zinazowafanya kupanda usukani mwa ligi hiyo inayoshirikisha timu 18 msimu huu, Azam sasa wako katika nafasi ya pili.

MCHEZO WENYEWE

Timu hizo ziliingia kwenye mchezo huo zikiwa na pointi sawa, ambapo kila moja ilikuwa na pointi 25, lakini Azam walikuwa kileleni wakiongoza kwa wingi wa mabao ya kufunga huku timu hizo zikutana kwa mara ya kwanza msimu huu katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo vikosi vyote viwili vilisheheni wachezaji wengi wa kigeni waliokuwa wanashindana kwa kucheza soka safi eneo la kati, lakini kosa moja lililofanywa na safu ya ulinzi ya Azam kwa kushindwa kumkaba Deus Kaseke ndio liliwagharimu na kujikuta wakifungwa.

Kaseke aliyeng’ara kwenye mchezo huo, alitumia makosa ya walizi hao kwa kuunganisha mpira moja kwa moja wavuni akipokea pasi ya Yacouba Sogne. Bao hilo lilionekana kuwanyong’onyesha Azam waliokuwa wenyeji wa pambano hilo ambalo kimsingi walihitaji ushindi ili kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo kwenye uwanja wao wa nyumbani.

USHINDANI MKALI

Pia kwenye ligi hiyo hadi sasa imeingia kwenye raundi ya 12 bado timu nyingi zimekuwa zikionesha ushindani mkali kwa kuonesha kandanda safi kujitengenezea mazingira ya kubaki nafasi za juu kwenye msimamo huo.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wanashika nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya pointi pointi 23 baada ya kucheza michezo 11, lakini hawakushuka dimbani juzi kutokana na kukabiliwa na michuano ya kimataifa wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Plateua ya Nigeria.

Kwa wastani kama Simba itacheza mchezo wake wa kiporo na akashinda, basi watamshusha Azam, kwani watakuwa wamefikisha pointi 26 na kutengeneza utofauti wa alama moja, huku Yanga akiendelea kuongoza.

Kwa ushindani wa mbio za ubingwa msimu huu kwa timu za Simba, Yanga na Azam matokeo yoyote mabaya yatakuwa na hasara kwa klabu husika na itakuwa nafasi nzuri kwa mpinzani kusonga mbele kwa kutengeneza uwiano mkubwa wa pointi.

Simba hadi sasa wanashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi wakipachika 29,wakifuatiwa na Azam 18 kisha Yanga wenye 14 ni wazi kwenye kila hatua inaweza kumnufaisha kulingana na ushindani unavyozidi kujionesha hadi mwishoni mwa ligi hiyo.

Ruvu Shooting wanashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo huo wakiwa na pointi 22, ni timu ambayo ilianza ligi kwa kusuasua kwa kupata sare nyingi lakini kocha wa kikosi hicho Charles Mkwasa alifanyia kazi changamoto ikiwemo kwenye sehemu ya ushambuliaji.

Maafande hao kwa sasa wamefanya vizuri kwenye michezo mitano mfululizo, kwani wameshinda michezo sita, sare nne na kupoteza michezo miwili hali inayowafanya kuwa timu tishio kwa kuwapa presha vigogo Simba, Yanga na Azam.

Polisi Tanzania wanakalia nafasi ya tano kwenye msimamo huo, wakiwa na pointi 19 walizojikusanyia baada ya kucheza michezo 12 wakishinda michezo mitano, sare minne na kupoteza mitatu. Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Malale Hamsini ,kinaonekana kuwa na wachezaji bora ingawa wamekosa muendelezo wa kupata ushindi.

Mfano, kwenye michezo yao mitano iliyopita wameshinda miwili na sare mbili na kupoteza mchezo mmoja ni wazi wanahitaji kutafuta sababu inayowafanya wachezaji wao kushindwa kulinda kasi yao.

Timu zinazoshika nafasi ya sita hadi 10 kila mmoja wao kama atashinda michezo miwili mfululizo wanaweza kupanda nafasi zaidi ya mbili kutokana na kwamba hazina muendelezo wa kupata matokeo mazuri.

KMC, Biashara United, Tanzania Prisons, Gwambina FC na Namungo FC kila timu inamzidi mwenzake pointi mbili au moja, mtiririko huo unaifanya ligi hiyo kugawika kwenye makundi matatu, zinazopigania nafasi ya ubingwa, waliopo katikati ya msimamo na waliopo katika hatari ya kushuka daraja.

Ingawa ni mapema mno kujua nani atashuka na nani atatwaa ubingwa, lakini siku zote biashara ni asubuhi na jioni ni jumuku la kuhesabu mapato. Mbeya City, Mwadui FC na Ihefu FC wapo kwenye nafasi hatarishi ingawa ishindani unazidi kuongezeka. Ihefu inayonolewa na Kocha Zuberi Katwila inashika mkia, ambapo tangu ligi hiyo imeanza wameshinda mchezo mmoja tu kati ya michezo 12 waliyocheza na wanapointi zao sita tu baada ya kushuka dimbani mara nane na sare tatu.

Kikosi hicho kinachangamoto ya kuwa na wachezaji wengi ambao hawana uzoefu na mechi za Ligi Kuu haki inayosababisha kushindwea kumudu misukosuko wanapokutana na uzoefu, ambap wanatakiwa wakati wa dirisha dogo kufanya usajili ili kujiimarisha. Mwadui wanakalia nafasi ya 17 wana pointi 10 sawa na Mbeya City , lakini wanatofautiana nafasi kwa uwingi wa mabao waliyofunga kama mmoja wao atashinda mchezo unaokuja na mwingine ikatokea amepoteza, basi matokeo yatamnufaisha mwenzake.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi