loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TFF, Simba na Yanga badilikeni soka la Tanzania likue

IFIKE wakati viongozi wa Simba na Yanga wakubali matokeo ya uwanjani, kufanya hivyo kunaweza kuthibitisha weledi wao na timu wanazoziongoza.

Asilimia kubwa ya viongozi wanaoziongoza timu hizo walianza kuzipenda timu na baada ya hapo ndio wakaja kuupenda mpira wenyewe ndio maana hawaendani na mfumo uliopo katika uendeshaji soka nchini.

Lakini wengine wapo kwa ajili ya maslahi yao na nia zao mbalimbali wengine kuchaguliwa na wanachama inapotokea uchaguzi wengine mambo ya siasa.

Ndio maana licha ya ukongwe na ukubwa wa timu hizo mpaka leo bado zinaendeshwa kwa kutegemea pesa kutoka mfuko wa mtu mmoja hazina vyanzo sahihi vya kuziendesha kama inavyotakiwa. Ukiyafutilia haya hautoshangaa pindi timu inapotokea kupoteza mechi kiongozi mmoja anajitokeza na kuwatupia lawama wachezaji au waamuzi kwamba wamehujumiwa.

Sulala la rushwa kwa klabu hizi linaanzia kwa viongozi wenyewe ambao kusudio lao kubwa ni kuona wanapata matokeo kwa njia zisizo halali na inapotokea tofauti basi wanawaza hujuma.

Hivi Duniani kuna timu gani ambayo haifungwi au kutoka sare, kwa kawaida jibu itakuwa hakuna swali la msingi inakuaje kiongozi mkubwa unajitokeza mbele za vyombo vya habari na kuwatupia lawama wachezaji kwamba wamehongwa na timu pinzani. Kadri miaka inavyokwenda mpira wa Tanzania umezidi kupoteza mwelekeo zamani haikuwa rahisi kusikia mambo ya hujuma kama hizi na timu yoyote iliweza kutwaa ubingwa mbele ya Simba na Yanga.

Timu kama Coastal Union, Majimaji, Cosmpolitani, Mecco, Mtibwa Sugar na Tukuyu Stars ziliweza kutamba na kutwaa ubingwa miaka ya nyuma mbele ya Simba na Yanga hii iliwezekana kutokana na uwepo wa haki na usawa kwa timu zote.

Lakini leo ni nadra sana kuona Yanga au Simba ikachezeshwa mechi mfululizo za ligi eti sababu kubwa ni kuwachosha wachezaji kutokana na ukubwa wa mchezo fulani uliopo mbele yao.

Maamuzi haya hufanywa kwa Yanga na Simba tu ndio maana kuna timu ambazo zimejipambanua kuwa ni shindano kama ilivyo Azam, lakini msimu wa 12 hazijafanikiwa wala kueleweka kwa mashabiki imefika wakati sasa hata matajiri wanatamani kuvunja timu sababu lengo walilotarajia bado lipo mbali. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi wanahusika katika kuzipa kichwa hata kupangua ratiba mara kwa mara na kuminyia baadhi ya mambo ya msingi kutokana ndani yao wapo viongozi wenye maslahi na timu hizo.

Kuwepo wao ndani ya shirikisho hilo ndio maana leo mikataba ya wachezaji inavuja, baadhi ya kesi kutoka upande mmoja zinashindwa kutolewa maamuzi haraka au kufunikwa hiyo ni kutokana na maslahi binafsi yaliopo kwa baadhi ya viongozi wa TFF.

TIMU ya soka ya Yanga Princess imezidi kujikita kileleni baada ...

foto
Mwandishi: Mohammed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi