loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ataka utafiti zaidi mapato na matumizi kaya binafsi

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), Dk Albina Chuwa amemtaka meneja wa takwimu za jamii katika ofisi ya serikali kuwahoji wananchi zaidi kuhusu utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi.

Alitoa mwito huo mkoani Manyara alipokutana na timu ya wataalamu wa ofisi hiyo na wizara wanayoandaa taarifa ya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi ya mwaka 2017/18. Alifanya ziara kukagua mwenendo wa uandaaji wa takwimu hizo kulingana na wananchi waliohojiwa katika kaya zao kuhusiana na jinsi wananufaika na huduma za kijamii kama vile maji, afya na elimu.

“Ripoti hii ya uandishi wa mapato na matumizi wa kaya binafsi tumeamua kuifanyia hapa Manyara kwa sababu bado tuna taarifa nyingine ambazo lazima tukazifanye kwa wanakaya na lazima twende kwenye kaya kwa ajili ya kuhakiki zile taarifa kabla hatujaziweka kwenye kitabu chetu kizima,” alisema Dk Chuwa.

Alisema baada ya kuwahoji zaidi wananchi kuhusu huduma mbalimbali upatikanaji wake kama vile maji na shule lengo ni ripoti itakapotoka isiwe ya kinadharia bali iwe na vitendo kwamba wananchi nao wameongea.

Amewataka wataalamu wanayofanya ripoti hiyo kuhakikisha inakamilika kabla ya Desemba mwaka huu, kwani kazi hiyo ndiyo itawasaidia kwa upana kwa serikali ambayo inaendelea mpaka 2025.

“Viashiria vipo mpaka sasa na tuna hali halisi wananchi wamezungumza nini, tumeshakamilisha data na maoni tuliyokusanya kwa wananchi wetu ili tuweze kujua tunafanyaje ili tuweze kwenda vizuri zaidi,”aliongeza.

Alisema kitabu hicho cha takwimu kitatoka kwa lugha ya Kiswahili na Kingereza ili mwananchi wa kawaida aweze kusoma na kuelewa kwani kiu ya wizara ni mwananchi wa kawaida aweze kutumia taarifa hizo katika kupanga mipango yake ya maendeleo.

Meneja wa takwimu za jamii katika ofisi hiyo, Silvia Meku alisema kulingana na uandaaji wa ripoti hiyo imefikia hatua ya rasimu.

Alisema ofisi ya taifa ya takwimu kwa kipindi cha mwaka 2017/18 ilitekeleza utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi kwa Tanzania bara ambao ulihusisha taarifa za mtu mmoja mmoja na taarifa za kaya kuhusu mapato na matumizi ambapo walikusanya taarifa za elimu, nguvu kazi, afya na elimu.

Dk Chuwa alisema kazi ambayo wanafanya Manyara kwa sasa ni kukamilisha uandishi wa ripoti kubwa yenye taarifa za kina za utafiti wa mapato na matumizi kwa kaya

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi