loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakenya waandaliwa ongezeko la kodi

WANANCHI wa Kenya wametakiwa kujiandaa kwa ongezeko la kodi na kupanda bei kwa bidhaa muhimu kama chakula na mafuta kuanzia mwakani kutokana na kadhia ya virusi vya corona.

Waziri wa fedha wa nchi hiyo, Ukur Yatani alisema kodi inayotozwa kwenye mishahara kuanzia mwakani itarejea katika kiwango cha kawaida cha asilimia 30, kutoka asilimia 25 iliyopunguzwa na serikali kutokana na janga la corona.

Kodi hii ilipunguzwa ili kutoa ahueni kwa mamilioni ya wafanyakazi nchini humo ili waweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na covid 19. Serikali pia inatarajiwa kurejesha kodi ya thamani kwenye bidhaa kwa asilimia 16 kutoka asilimia 14 iliyokuwa imepunguzwa na serikali ili kupunguza makali ya athari ya corona.

Yatani alisema kurejesha tozo za awali kunalenga kuisaidia serikali kuongeza ukusanyaji mapato. Aidha waziri Yatani, amezitaka wizara na taasisi nyingine za serikali kujiandaa na makali yatakayoshuhudiwa, ambapo serikali inalenga pia kupunguza baadhi ya bajeti za wizara na taasisi ili kufidia ombwe lililopo sasa.

Haya yanajiri wakati huu kamati ya bunge ikitarajiwa kujadili ripoti ya uchunguzi kuhusu sakata la matumizi mabaya ya fedha za kukabiliana na janga la Corona katika ofisi ya manunuzi ya dawa za Serikali (Kemsa)


WANASHERIA  wa Aliyekuwa Mgombea wa Urais nchini Uganda ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi