loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pele: Tutacheza pamoja juu mawinguni

GWIJI wa soka duniani, Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’ ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba wa nahodha na kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, Diego Armando Maradona.

Maradona alifariki dunia juzi akiwa na umri wa miaka 60, na taarifa za kifo chake zilithibitishwa na Shirikisho la Soka, Argentina kupitia kwa Rais wake Claudio Tapia.

Pele alituma salamu za rambirambi akisema, “Pengine siku moja tutacheza pamoja mpira juu mawinguni,” alisema Pele katika taarifa yake fupi iliyotolewa na wawakilishi wake na ikinukuliwa na Shirika la habari la Reuters. Maradona hivi karibuni alikuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya huku akilazwa mara kadhaa.

Jumatano, akiwa nyumbani kwake jijini Buenos Aires, mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 1986 akiwa na Argentina alifariki dunia kwa mshtuko wa moyo.

Rais wa Argentina, Alberto Fernandez alitangaza siku tatu za maombelezo ya kitaifa kutokana na kifo hicho Mapema mwezi huu, nyota huyo alifanyiwa upasuaji wa ubongo kwa ajili ya kutoa damu iliyokuwa imeganda na baadaye akaruhusiwa kutoka hospitali. Baada ya upasuaji huo, ilitangazwa kuwa Maradona angeanza matibabu ya uraibu wa pombe.

Katika kukiweka kikosi katika hali ya ushindani, Arsenal ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi