loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shilole kuja na lebo yake

MSANII wa Bongo fl eva , Zuwena Mohammed ‘Shilole’ametambulisha lebo yake mpya inayoitwa Shishi Gang, pamoja na wasanii watakaounda kundi hilo. Akizungumza Dar es Salaam juzi, Shilole alisema lebo hiyo itakuwa inashughulika na mambo mengi na siyo muziki tu kama watu wanavyotarajia.

“Natambulisha rasmi lebo yangu ya’ Shishi Gang’ ambayo kimsingi itakuwa inaundwa na wasanii wengi tutakaokuwa tunafanya kazi kwa kushirikiana kama yanavyofanya makundi mengine ya muziki,” alisema Shilole.

Shilole anayetamba na vibao kadhaa ikiwemo cha Ukintekenya, Pindua meza na mtoto mdogo alimtangaza msanii Clayton Chipando ‘Baba Levo’ kuwa msemaji wa lebo hiyo ambayo anaamini itafanya vyema kwenye soko la muziki nchini.

Alisema hana mambo mengi ya kuwaletea mashabiki wake zaidi ya kuendelea kuwapa kazi nzuri na ameanzisha lebo hiyo kwa lengo la kuwanyanyua wasanii chipukizi na kukuzwa kwenye kundi hilo.

Shilole ni msanii wa kwanza wa kike kumiliki lebo yake hapa nchini akifuata nyayo za mastaa kama Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayemiliki WCB na Ali Kiba mwenye ‘King’s Music Record’ na Rajab Abdul ‘Harmonize’ anayemiliki Konde Gang

MTOTO Juma Megejuwa (12) mkazi wa ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi