loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaume watajwa kuathirika rushwa ya ngono vyuoni

WANAFUNZI wa kiume katika taasisi za elimu ya juu wametajwa kuwa pia huathirika kutokana na madhara ya rushwa ya ngono.

Hayo yamebainika jana katika kongamano la maad- himisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili Duniani lililoan- daliwa na Mtandao wa Kupinga Rushwa ya Ngono nchini Tanzania na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia utafiti wa rushwa ya ngono katika taasisi za elimu ya juu uliopewa jina la Uchunguzi Kifani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dodoma, Ofisa wa Takukuru, Denis Lekayo alisema rushwa ya ngono mahali pa kazi katika taasisi za elimu vikiwamo vyuo vikuu, huwaathiri pia wanafunzi na wafanyakazi wa kiume kwa kuwekewa sharti la ngono ili kupata huduma. 

“Akina mama na nyie msitumie mamlaka yenu kuweka kigezo hicho cha kufanya umalaya na vijana ili kutoa huduma. Mfano, baadhi ya wahadhiri katika elimu ya juu huwawekea wanafunzi masharti magumu ili kuwezesha wenzao kupata rushwa ya ngono kwa wanafunzi na pia,” alisema Lekayo.

Alisema wakati wa utafiti shuhuda zilizotolewa zilibainisha kuwapo wanafunzi wa kike waliofelishwa kutokana na kukataa rushwa ya ngono, au wanafunzi wa kiume waliofelishwa kwa vile marafiki wao wa kike walikataa kutoa rushwa ya ngono.

“Rushwa ya ngono husababisha kuwapo wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu zikiwamo za vyuo vikuu wakiwa na vyeti feki kwa kuwa gradi zilizo katika vyeti haziendani na kilicho kichwani,” alisema.

Alisema katika mada ya Mrejesho wa Utafiti Uliofanywa na Takukuru Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma Kuhusu Hali Halisi ya Rushwa ya Ngono katika vyuo vikuu nchini kuwa, licha ya vyuo vilivyohusika katika utafiti kuwa na sera, miongozo na sheria ndogondogo zinazoharami- sha rushwa ya ngono, bado tatizo hilo ni kubwa katika vyuo vikuu hivyo.

Kwa mujibu wa ofisa huyo wa Takukuru, miongoni mwa mbinu zinazotumika kudai rushwa ya ngono vyu- oni ni pamoja na wahadhiri kutoa alama za chini katika mitihani, huku wengine wakiwaahidi wafanyakazi kuwapa ufadhili wa masomo yakiwamo ya nje ya nchi kwa ngazi za juu.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake katika Sheria na Maendeleo (WiLDAF), Anna Kulaya, alisema rushwa ya ngono huathiri pia wanafunzi wa kiume hasa wenye urafiki na wanafunzi wa kike wanaodaiwa rushwa hiyo.

Alisema changamoto kubwa katika vita ya rushwa ya ngono ni wahusika kukwepa kutoa ushahidi katika vyombo vya sheria.

Katika ufunguzi wa kongamano hilo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Aseny Moro alisema rushwa ya ngono ni tatizo kubwa nchini linalompora haki mwanamke kwa kumvua utu wake mbele ya jamii.

“Tunajivunia serikali yetu kwa kulifanya suala la ku- pambana na rushwa ya ngono kuchukuliwa na serikali katika mipango yake...,” alisema.

Alitaka kuwapo kwa mfumo unaowalinda wa- fanyakazi au wanafunzi wanajikuta katika mazingira magumu kwa kutoa taarifa dhidi ya rushwa ya ngono.

“Hivi unafikiri hata kama walimu wataungana na kumfanyia visasi mwanafunzi huyo, serikali haishindwi kuwaondoa wote na kuajiri wengine ili liwe fundisho,” alihoji.

Kwa upande wa wanafunzi, ripoti inashauri wa- ongeze jitihada katika masomo, wazingatie maadili, wasikubali kurubuniwa, wavunje ukimya na kupaza sauti kunapotokea viashiria vya kuwanyima haki zao na wachukue hatua stahili wanapopokonywa haki hizo na kufikisha malalamiko yao Takukuru kupitia kamati zao, taasisi za kiraia na wao wenyewe.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi alisema huu ni utafiti mzuri na wenye manufaa makubwa kwa taifa uliofanywa na serikali kupitia Takukuru.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi