loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gesi asilia yaokoa trilioni 33/- za nishati

JUMLA ya Sh trilioni 33 zimeokolewa na kuelekezwa katika matumizi mengine kutokana na mchango wa gesi asilia kwenye uchumi wa taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji wa Petroli nchini (TPDC), James Mataragio alisema hayo jana jijini hapa kwe- nye warsha ya siku nne inayo- husisha wataalamu wa sekta ya madini, wanasayansi na wachim- baji wadogo.

Akizungumzia mchango wa sekta ya gesi katika kukuza uchumi kwenye warsha hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Jiolojia Tanzania( TGT), alisema pia wamelipa takribani Sh bilioni 600 za kodi mbalimbali kutokana na mauzo ya gesi asilia.

Alisema TPDC imerejea katika biashara ya mafuta na bidhaa zake kupitia kampuni tanzu ya TANOil ambayo iliundwa kwa mujibu wa Sheria, lengo likiwa ni kuendesha biashara hiyo.

“Hadi sasa TPDC kupitia kampuni hiyo tumefanikiwa kutwaa maeneo katika mikoa ya Tanga, Dodoma na Dar es Salaam kwa lengo la kujenga maghala ya kuhifadhi mafuta ya kimkakati,” alisema.

Alisema, ndani ya miaka mitano ijayo, TPDC inatarajia kujenga vituo vya mafuta 100 nchi nzima kwa kushirikiana na halmashauri mbalimbali na sekta binafsi.

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo yote utaifanya Tanzania kuwa kituo kikuu cha nishati na kuhu- dumia nchi za Afrika Mashariki na Kati. Pia itakuza viwanda vya ndani na kuongeza fursa za ajira pamoja na kuchangia pato la taifa.

“Hadi sasa tuna maombi kadhaa kutoka nchi jirani kama vile Zambia, Kenya na Uganda na hivyo jukumu letu ni kuchangamkia fursa hii,” alisema.

Alisema pamoja na utekelezaji wa miradi ya kipaumbele, imeende- lea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati.

Alisema kwa miaka ya hivi karibuni imefanikiwa kukusanya takwimu mbalimbali katika vitalu vya Eyasi Wembere, Songosongo Magharibi, Mnazi Bay Kaskazini na Ziwa Tanganyika kwa lengo la kuongeza thamani ya vitalu.

“Takwimu hizi zinapatikana na zinaweza kutumika katika utafutaji wa madini na gesi aina ya helium,” alisema.

Alisema katika kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini, wamejipanga kuchimba visima viwili katika mwaka huu wa fedha kwa kutumia fedha za ndani, ambavyo vitakuwa vya utafutaji na uhakiki.

“Na matarajio yetu ni kugundua gesi asilia kwa mujibu wa taarifa za awali ambazo zinaonesha eneo lile kuzungukwa na ugunduzi mbalim- bali za gesi asilia na gesi nyingi,” aliongeza.

Alisema pamoja na miradi ya utafutaji wa gesi, TPDC imeendelea kuzalisha gesi asilia kwa kushiriki- ana na wabia wake, Pan African Energy na Maurel and Prom katika vitalu vya Songo Songo na Mnazi Bay.

“Uzalishaji wa gesi umekua kwa asilimia 100 katika kipindi cha miaka mitano kutoka futi za ujazo milioni 100 kwa siku mwaka 2015 hadi futi za ujazo milioni 200 kwa siku,” alisema.

Alisema hadi sasa mteja mkubwa wa gesi asilia ni Shirika la Umeme (Tanesco) ambalo asilimia 60 ya umeme unaozalishwa katika gridi ya taifa unatokana na gesi asilia.

“Mbali na kuzalisha umeme, gesi asilia pia inatumika katika viwanda vipatavyo 48 hapa nchini, nyumba takribani 500 na magari zaidi ya 400,” alisema.

Akifungua warsha hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alipongeza Chama cha Jiolojia Tanzania kwa mchango wao katika ukuaji wa uchumi. Alisema katika kipindi cha miaka mitano pekee kumekuwapo na mafanikio makubwa kwenye sekta ya madini.

Rais wa TGS, Profesa Ab- dulkarim Mruma alipongeza juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli kwenye sekta ya ma- dini ambayo imedhihirishia dunia kwamba Tanzania imefanya udhibiti mkubwa katika sekta hiyo na kuleta tija kwa nchi katika ukuaji wa uchumi wake.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi