loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tozo ya sasa ya kuzidisha uzito kukoma Desemba

VIWANGO vya tozo ya kuzidisha uzito wa magari vya sasa vinatarajiwa kukoma mwishoni mwa mwezi ujao kabla ya vipya kuanza Januari Mosi mwakani.

Taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi) iliyotolewa jana imesema ukomo wa viwango vya sasa ni Desemba 31 mwaka huu.

Hii ni kwa mujibu wa sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Udhibiti wa Uzito wa magari ya mwaka 2016 na kanuni zake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa wizara, viwango hivyo vitatumika kama vilivyoainishwa katika jedwali la tatu la kanuni za taratibu za usimamizi za mwaka 2018.

Aidha taarifa hiyo ilifafanua kuwa sheria na kanuni zinazohusu viwango vipya vya tozo za kuzidisha uzito wa magari zinapatikana kupitia tovuti ya wizara. “Kwa taarifa hii, napenda kuwahimiza na kuwashauri wadau wote kujiandaa kwa utekelezaji wa mabadiliko hayo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi