loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DIEGO MARADONA: MKONO WA MUNGU NA BAO LA KARNE

DIEGO Maradona atakumbukwa kwa mechi aliyofanya wakati wa uhai wake yakiwemo mabaya na mazuri ndani na nje ya uwanja.

Maradona alifariki dunia Jumatano, ataendelea kukumbukwa kwa bao lake la mkono lililoipatia ushindi timu ya taifa ya Argentina ilipoifunga England katika robo fainali ya Kombe la Dunia.

Mchezaji huyo alikuwa mtata na pia mwenye mbinu nyingi uwanjani huku akifunga goli la mkono wa Mungu pamoja na bao la karne kutokana na ubora wa bao hilo.

Muargentina huyo alibadili kabisa Kombe la Dunia 1986. Ndiye alikuwa gumzo katika fainali hizo na alikuwa akikubalika hata na wachezaji wenzake, ambao wakati wote walikuwa wakimzunguka.

Nyota huyo wa Argentina aliiwezesha nchi yake kutoka hatua ya makundi na kuipeleka timu hiyo katika hatua ya mtoano na hatimaye mchezaji huyo alibeba taji la Dunia.

Fainali za Kombe la Dunia la mwaka 1986 ni kama mali ya Diego. Lakini ilikuwa robo fainali wakati Argentina ilipocheza dhidi ya England Jumapili, Juni 22 ambayo bado inabaki kuwa kumbukumbu katika historia yake ya soka. Hasa dakika hizo nne, ambazo zinamfanya gwiji huyo kukumbukwa milele. Joto lilikuwa kali Mexico City.

Wakati wa kuelekea mechi hiyo ya robo fainali dhidi ya England. UWEZO MKUBWA Maradona alikuwa mmoja wa wachezaji wenye uwezo mkubwa katika soka kwa kuweza kukimbia kwa kasi na mpira huku akipiga chenga tena zile za maudhi na kufunga mabao bora.

Vitendo hivyo kiujumla viliwafurahisha sana mashabiki na kuleta raha ndani ya mioyo ya wapenda soka wa Argentina na duniani kwa ujumla. Pia aliwakuna mashabiki kwa matendo ya utata, ikiwemo bao alilofunga kwa `Mkono wa Mungu’ huku akikumbwa na kashfa ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni pamoja na vurugu uwanjani.

RAHA NA TABU

Maradona alizaliwa miaka 60 iliyopita huko Buenos Aires katika eneo duni, ambako Diego Armando Maradona alikwepa umasikini wa hali ya juu aliokumbana nao utotoni kwa kuwa nyota mkubwa wa soka, huku wengine wakifikiri kuwa alikuwa zaidi ya Mbrazili Pele.

Muargentina huyo aliyefunga mabao 259 katika mechi 491, aliwapita wapinzani wao wa Amerika ya Kusini na kutangazwa mchezaji bora wa karne ya 20, kabla Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) halijabadili utaratibu wa kupiga kura, ambapo wachezaji wote walituzwa.

Maradona alionesha uwezo mkubwa tangu akiwa mdogo akiiongoza timu ya vijana ya Los Cebollitas kucheza mechi 136 mfululizo bila kufungwa na kuanza kucheza mechi za kimataifa akiwa na umri wa miaka 16 na siku 120. Umbo lake la futi 5.5, kwa kweli sio umbo la uchezaji, lakini yeye alifanya kweli pamoja na ufupi wake huo.

MKONO WA MUNGU

Mabao 34 ya Maradona katika mechi 91 aliyoichezea Argentina inaonesha sehemu ndogo tu ya mafanikio ya mchezaji huyo katika soka la kimataifa.

Mchezaji huyo aliiongoza nchi yake kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1986 wakati fainali hizo zilipofanyikia Mexico na kuipeleka timu hiyo katika fainali miaka minne baadae.

Mchezo huo wa robo fainali kati ya Argentina dhidi ya England uligubikwa na malumbano ya vita kati ya nchi hizo mbili katika visiwa vya Falklands ambayo ilifanyika miaka minne iliyopita.

Zikiwa zimechezwa dakika 51 na mchezo ukiwa suluhu, Maradona aliruka na kipa wa England, Peter Shilton na aliugonga mpira kwa mkono na kujaa wavuni.

Baadae alisema kuwa shukrani kwa goli kupatikana “kiasi fulani lilifungwa kwa kichwa cha Maradona na kidogo kwa mkono wa Mungu”.

Dakika nne baadae, mchezaji huyo kwa kutumia juhudi binafsi alifunga kwa kile kilichoelezewa bao la karne, baada ya kupata mpira akiwa upande wa timu yake na kukimbia nao huku akimpiga chenga mmoja baada ya mwingine na kuwafungisha tela kabla ya kumzunguka Shilton na kufunga.

Bao la kwanza lilikuwa la mashaka; la pili lilikuwa la ajabu kweli, alisema kocha wa zamani wa England Sir Bobby Robson.

“Unatakiwa kusema kuwa ni bao safi. Hakuna ubishi kuhusu goli lile. Kwa kweli yule ni mtu wa ajabu katika soka,” alisema mtangazaji wa BBC Barry Davies. England ilifunga bao ka kufutia machozi, lakini Argentina ilipenya, huku Maradona akisema “ilikuwa zaidi ya kushinda mechi, kikubwa kilikuwa ni kuitoa Uingereza”.

REKODI YA USAJILI

Maradona alivunja rekodi ya usajili mara mbili, wakati akiondoka Boca Juniors timu yake ya nyumbani kwao na kwenda Hispania katika klabu ya Barcelona, ambako alinunuliwa kwa pauni milioni 3 mwaka 1982 na pale alipojiunga na klabu ya Italia ya Napoli miaka miwili baadae kwa pauni milioni 5.

Kulikuwa na mashabiki zaidi ya 80,000 kwenye Uwanja wa Stadio San Paolo wakati Maradona akiwasili kwa helikopta. Shujaa mpya. Aliichezea klabu bora kabisa wakati akicheza soka nchini Italia, ambapo alivuta hisia za mashabiki na kufanya wampende sana na kutwaa taji la ligi mwaka 1987 na 1990 na Kombe la Uaya mwaka 1989.

Sherehe ya kushangilia ushindi huo ilifanyika kwa siku tano, huku maelfu ya mashabiki walijazana mitaani, lakini Maradona alisongwa na kutaka apatiwe nafasi ilia pate hewa vizuri.

“Hili ni jiji kubwa lakini nashindwa kupumua. Nataka kuwa huru kuzunguka…,” alisema.

KUSTAAFU SOKA

Baada ya vipimo vya mara ya tatu miaka mitatu baadae na kubainika kuitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, Maradona alistaafu kucheza soka wakati wa siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 37, lakini aliendelea kuandamwa na mikosi.

Maradona alifungwa jela miaka miwili na miezi 10 kwa tukio la awali baada ya kumpiga risasi mwandishi wa habari kwa bunduki aina ya rifle. Matumizi yake ya dawa za kulevya aina ya cocaine na matumizi makubwa ya pombe yalisababisha kupata matatizo tofauti tofauti ya kiafya, ambapo aliongeza uzito hadi kufikia kilo 128 na kupata shambulio kubwa la moyo mwaka 2004, na kumfanya kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Taarifa ikufikie kuwa wimbo wa ‘Destiny’ wa msanii ...

foto
Mwandishi: BUENOS AIRES, Argentina

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi