loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Usikilizaji, utekelezaji wa adhabu kesi za watoto ni changamoto

UKOSEFU wa miundo mbinu kwa ajili ya usikilizaji wa kesi zinazohusu watoto imekuwa changamoto kubwa inayokabili idara ya mahakama mkoani Kigoma.

Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa Kigoma, Gadiel Mariki alisema hayo akijibu maswali ya gazeti kutaka kujua athari zinazotokana na kutokuwepo kwa mahakama maalumu kwa ajili ya usikilizaji wa kesi zinazohusu watoto.

“Kwa sasa kesi zinazohusu watoto zinasikilizwa kwenye mahakama ya wilaya Kigoma lakini kwa kutumia vyumba vya mahakimu na siyo ukumbi wa wazi wa mahakama,” alisema.

Aliongeza, “Lakini bado haitoshi kuwa salama kwani wanapoingia na kutoka mahakamani bado watoto hao wanakutana na watuhumiwa ambao wamefungwa pingu na vitu vingine ambavyo watoto hawapaswi kuviona.”

Alisema pia ukosefu wa shule maalumu za mafunzo (jela za watoto) kunaathiri mienendo ya kesi za watoto wanaohukumiwa kwa makosa mbalimbali na hivyo kusababisha kutolewa kwa adhabu za viboko na vifungo vya nje jambo ambalo haliwi fundisho katika kujenga tabia na maadili kwa watoto.

Akizungumzia changamoto hiyo, Naibu Msa- jili wa Mahakama Kuu kanda ya Kigoma, Anold Kirekiano alisema kuwa kunahitajika ushirikiano wa pamoja wa kuona umuhimu wa kujenga shule za mafunzo za watoto na rumande ambazo watoto wenye kesi wanaweza kuwekwa wakisubiri mashauri yao.

Mwendesha Mashitaka wa serikali mkoa Kigoma, Riziki Matitu alisema kuwa kutokuwepo kwa shule za mafunzo hakuna athari katika utekelezaji wao wa kusimamia kesi na kuzipeleka mahakamani.

Akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha kamati kuu ya Mradi wa Pamoja Kigoma unaotekelezwa na mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), Sampath Perera anayesimamia mpango wa kupinga unyanyasaji kwa wanawake na watoto alisema kuwa jumla ya mashauri 481 yamepata msaada wa kisheria.

Kati yao, wanawake ni 201 na watoto 280. Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa Kigoma, Msafiri Nzunuri alisema kuwa tangu kuanza kutekelezwa kwa mradi wa pamoja Kigoma, polisi wameongeza umakini na ufuatiliaji katika kukamata na kusimamia kesi zinazohusiana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na watoto.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi