loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbio za hisani watu wenye ulemavu kuanza kesho

MAMIA ya wakazi wa jiji kesho wanatarajiwa kuungana na watu wenye ulemavu katika mbio za hisani (marathoni) zinazolenga kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu 2020.

Mbio hizo zilizoandaliwa na Taasisi inayojihusisha na utoaji wa misaada kwa Watu wenye Ulemavu ya Dk Mengi (DMRF), inakusudia kukuza uelewa wa umma juu ya aina tofauti za ulemavu.

Mbio hizo ziliyopewa jina la 'Walkathon' zinazotarajiwa kuyashirikisha makundi na kukimbia umbali kuanzia Km 5 hadi 25 zinatarajiwa kuanzia Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa DRMF, Shimimana Ntuyabaliwe alisema pamoja na mbio za miguu mbio hizo pia zinatarajiwa kuhusisha waendesha baiskeli watakaoendesha umbali wa Km 35 

"Natoa wito kwa wakaazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kushiriki  mbio hizo kwa lengo la kuonyesha upendo kwa  watu wenye ulemavu," alisema Ntuyabaliwe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika llinaloshughulika na watu wenye matatizo ya akili (TUSPO),  Pangarasi Msongore, alisema watatumia mbio maalumu za kesho kuielimisha jamii juu ya watu wenye matatizo ya akili.

"Afya ya akili ni muhimu sana kwa sababu  ndiyo inayotoa watu wenye elimu na wataalamu, hivyo ni vyema pia tukaitumia nafasi hiyo kuiasa jamii kuwa karibu na watu wenye walemavu wa akili"alisema Msongore

Naye Mwenyekiti wa chama cha waendeshaji baiskeli jijini Dar es Salaam, Haussein Ally alisema watashiriki mbio za marathon kusaidia DMRF kueneza uelewa juu ya ulemavu.

Hafla hiyo ni sehemu ya shughuli za wiki nzima kuadhimisha Siku hiyo ambayo inaadhimishwa ulimwenguni mnamo Desemba 3 kila mwaka.
Wakati wa Siku hii, maadhimisho ya kila mwaka ya watu wenye ulemavu, ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa Mwaka huu anasema  'Siyo Walemavu Wote Wanaonekana' inapaswa kueneza ufahamu na uelewa wa ulemavu ambao hauonekani mara moja.

Kulingana na Ripoti ya Ulimwengu ya Ulemavu ya WHO, asilimia 15 ya idadi ya watu ulimwenguni, au zaidi ya watu bilioni 1, wanaishi na ulemavu.

Kati ya idadi hiyo, inakadiriwa kuwa milioni 450 wanaishi na hali ya ulemavu wa akili au ukosefu wa ufahamu ambapo theluthi mbili ya watu hao huitaji msaada wa matibabu, kwa sababu ya unyanyapaa, ubaguzi na kupuuzwa.
 

TIMU ya soka ya Yanga Princess imezidi kujikita kileleni baada ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi