loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mume. Mke wakutwa na kesi ya kujibu usafirishaji wa Mihadarati

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi imewakuta na kesi ya kujibu mfanyabiashara Ayubu Kiboko na mke wake Pilly Kiboko wanaokabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine gramu 251.25.

Hatua hiyo imefikiwa mahakamani hapo Novemba 26,2020, baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao katika kesi hiyo kwa kupeleka mashahidi sita na vielelezo 16 yakiwemo magari matatu aina ya Toyota Prado, Toyota Hilux na Toyota  Land Cruiser.

 Baada ya kufunga ushahidi kwa shahidi wa mwisho aliyetambulishwa mahakamani hapo kwa jina la Raymond Kimambo ambaye ni jirani wa Kiboko, Jaji Mashaka amesema upande wa mashtaka wameweza kuthibitisha kuwa washtakiwa wana kesi ya kujibu.

"Upande wa mashtaka wameweza kuthibitisha kuwa kuna kosa wametenda washtakiwa, kwa hiyo wamepatikana na kesi ya kujibu. Mnahaki ya kutoa utetezi wenu chini ya kiapo na pia mna haki ya kuleta mashahidi wengine," amesema Jaji Mashaka.

Katikabhali isiyotarajiwa baada ya Jaji kuwatia hatiani mahakama imeshuhudia mshtakiwa namba mbili akiangua kilio lakini Jaji Mashaka amemsihi anyamaze na ajiandae kwa ajili ya kijitete.

" Nakuomba usilie, hapa mmekuja kutafuta haki, unatakiwa ujipange uje ujitetee, ukilia sasa hivi haitasaidia, jipange utoe utetezi wako," 

Washtakiwa hao kupitia wakili wao Majura Magafu, wamedai kuwa watajitetea kwa kiapo, na kuahidi kuleta kadi halisi za magari yaliyowasulishwa kama vielelezo mahakamani.

 Naye Wakili wa Serikali Salim Msemo anayewakilisha Jamhuri sambamba na Wakili wa Serikali Constantine Kakula na Candid Nasua, ameomba mahakama iridhie gari zilizokamatwa zibaki chini ya Mamlaka ya Dawa za Kulevya (DCEA) na Jaji akaridhia kwa kuyakabidhi kwa Inspekta Hassan Msangi.

"Ninamkabidhi Inspekta Hassan Msangi kielelezo P13, P14 na P15 kwa ajili ya kuhifadhi na anatakiwa kuyaleta jumatatu. Washtakiwa mtaendelea kuwa nchini ya uangalizi, mjiandae mje mtoe utetezi wenu,"  

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 29 ya mwaka 2018 Kiboko na mkewe wanakabiliwa na shtaka moja ambapo wanadaiwa kusafirisha dawa za kuĺevya aina ya Heroin zenye uzito wa gram 251.25 kosa wanalodaiwa kulitenda Mei 23, 2018 eneo la Tegeta Nyuki Masaiti wilaya ya Kinondoni.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi