loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbunge Ulega kutembelea miradi Mkuranga

MBUNGE  wa Mkuranga Abdallah Ulega anatarajiwa kufanya ziara ya siku nne kutembelea miradi mbalimbali iliyopo katika jimbo hilo kuangalia utekelezaji wake.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge huyo,  ziara hiyo inatarajiwa kuanza Jumatatu ya wiki ijayo ikihusisha maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mkuranga.

Taarifa hiyo imesema kuwa Jumatatu ya mwanzo wa wiki, Ulega anatarajiwa 
kutembelea kiwanda cha madawati kwa Mkuu Wilaya hiyo, Ujenzi wodi ya wazazi unaoendelea katika hospitali ya wilaya Mkuranga pamoja na ujenzi wa tanki la maji katika eneo la Mkwalia unaoenda sambamba na  ujenzi wa Pump. 

Aidha ratiba hiyo inaonyesha kuwa Jumanne Ulega anatarajiwa kutembelea miradi ya ujenzi wa Shule ya Msingi Chatembo, ujenzi wa kituo cha afya cha Vikindu pamoja na  ujenzi wa Zahanati ya Mwandege .

Pamoja na maeneo hayo,  ratiba hiyo imenyesha kuwa siku hiyo Mbunge huyo atatembelea Barabara ya vikindu Vianzi na daraja la Sangatini, daraja la Mipeko pamoja na daraja la Kifaurongo.

Ziara hiyo ya Mbunge huyo inakuja katika kipindi kisichozidi wiki mbili tangu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania awaapishe wabunge wa Bunge jipya la 12 mara baada ya kumalizika kwa mchakato wa uchaguzi Mkuu uliofanyika oktoba 28 Mwaka huu.

Aidha akizungumza ziara hiyo, Ulega alisema ziara hiyo ni imelenga kupata ufumbuzi wa haraka wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo lake ikiwa ni utekeleza wa ahadi mbalimbali alizozitoa kipindi cha kampeni. 

Alisema kwa sasa kazi iliyopo mbele yake ni kuhakikisha kero zote ambazo zimeanishwa na wananchi katika jimbo hilo zinatatuliwa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais John Magufuli.

MTOTO Juma Megejuwa (12) mkazi wa ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi