loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hazard aumia tena Real ikifungwa

EDEN Hazard ameumia tena wakati Real Madrid ikipokea kichapo cha mabao 2-1 nyumbani kutoka kwa Alaves katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga.

Hazard, ameanza mara tatu tu katika mechi za ligi msimu huu na ni mara ya nne ameanza katika mashindano yote, alitolewa nje dakika 28 tangu mchezo kuanza baada ya kuumia mguu.

Penalti ya dakika ya tano ya Lucas Perez iliifanya Alaves kuwa mbele baada ya mpira wa kichwa uiliopigwa na Victor Laguardia, ambao uligonga mkono wa Nacho na kuwa penalti.

BAHATI MBAYA

Hazard, 29, alijiunga na Real Madrid akitokea Chelsea kwa ada ya Pauni milioni 150 mwaka 2019.

Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amecheza mechi 27 katika kikosi cha Zidane tangu ajiunge kwa gharama hiyo kubwa.

Hazard alikosa mwanzo wa msimu kutokana na maumivu ya misuli upande wa mguu wake wa kulia na alifanikiwa kucheza mara tatu kabla ya kupimwa na kukutwa na virusi vya corona mwanzoni mwa Novemba.

Tangu wakati huo alianza katika mchezo dhidi ya Villarreal Novemba 21 na alifunga penalti Jumatano katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Inter Milan, akicheza dakika 65 na 78 katika echi hizo zote.

Lakini mshambuliaji huyo alidumu chini ya nusu saa katika mchezo huo wa Jumamosi, akiumia tena mguu katika usiku ambao haukuwa mzuri kwa vijana hao wa Real Madrid katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Alfredo di Stefano.

"Eden, nafikiri na ninatumaini ameumia kidogo. Hicho ndicho alichotuambia. Ameumia kidogo, sio misuIi, “alisema kocha Zidane baada ya kipigo hicho.

Wenyeji waliuanza mchezo huo bila ya kuwa na wachezaji wake muhimu kama nahodha Sergio Ramos na mshambuliaji Karim Benzema na kufaya kukosa uimara katika ulinzi na ushambuliaji, wakati kocha Zidane pia alikuwa na majeruhi Dani Carvajal na Federico Valverde.

Ikiwa imechapwa mara tatu, Real imefungwa mara nyingi msimu huu baada ya mechi 10 kama walivyofanya walipocheza mechi 38 katika msimu wa mwaka 2019-20 walipotwaa taji la La Liga.

Jumannre wataifuata Shakhtar Donetsk katika mchezo wa Ligi ya Mabigwa wa Ulaya hatua ya makundi, ambapo ushindi utaiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Baadae Joselu alifunga katika lango lililokuwa wazi baada ya pasi mbovu ya kipa Thibaut Courtois kabla Casemiro hajafunga bao la kufutia machozi kwa Real Madrid.

Mchezo huo watatu bila kikosi hicho cha Real Madrid chini ya kocha Zinedine Zidane kushinda na kuaicha timu hiyo ikiwa katika nafasi ya nne ya msimamo wa La Liga, pointi sita nyuma ya vinara Real Sociedad na  Atletico Madrid na mbili nyuma ya Villarreal iliyopo katika nafasi ya tatu.

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi