loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Polepole na Lulida wala kiapo

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai leo Novemba 30   amewaapisha wabunge wawili kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole na Riziki Lulida walioteuliwa na rais Dk John Magufuli  katika viwanja vya bunge Dodoma

Wabunge hao wameteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 66 (1) (e)  ya Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayompa mamlaka rais kuteua wabunge wasiozidi kumi kutoka katika watu wenye sifa za kuwa wabunge.

Wabunge hao wanaungana na wabunge wengine 264 pamoja na wabunge 19 kutoka chama cha Chadema walioapishwa hivi karibuni.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa  Polepole   amesema kuwa kupitia eteuzi huo atahakikisha anamsaidia Rais Dk John Magufuli kusimamia ipasavyo yale yote  aliyohaidi   kipindi cha kampeni    yawe uhalisia kwa wanachi.

Kwa upande wake  Riziki Lulida alimshukuru Rais Magufuli kwa kuwa na imani naye hadi kumteua kushika wadhifa huo pamoja na  kutoa ahadi ya kuchapa kazi kwa bidii ili asiweze kumuangusha.

JESHI la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Said Shabani ...

foto
Mwandishi: ALFRED LUKONGE

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi