loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaotoroka mgambo kukiona cha moto

 Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, Lauteri Kanoni amesema kuwa serikali ipo  mbioni kuandaa utaratibu kwa wale wote wanaojiunga na mafunzo ya jeshi la akaiba na kushindwa kumaliza kwa kutoroka kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwakuwa   tayari watakuwa wamefahamu mbinu za awali za kijeshi.

Kanoni amesema hayo kwenye mahafali ya jeshi la akiba yaliyofanyika katika kata ya Makoga wilayani humo na kuwaasa wahitimu kuwa wazalendo kwa nchi yao.
 

“Tunatengeneza utaratibu mtu akijiunga na mafunzo haya na kupata mafunzo ya awali ya kijeshi alafu akatoroka akamatwe kama muhalifu kwakuwa tayari atakuwa anajua baadhi ya siri za jeshi” amesema Kanoni.

Aidha, Kanoni ametoa agizo kwa halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha inatenga bajeti ya kununua mavazi kila mwaka kwa wanafunzi wa mafunzo hayo.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi