loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtanzania aliyehukumiwa kwa ugaidi Kenya ajinyonga gerezani

TANZANIA aliyefungwa jela maisha kwa tuhuma za ugaidi kutoka- na na kuhusika kwenye shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya, amekutwa amekufa kwa kujinyonga katika gereza la Kamiti nchini humo.

Mtanzania huyo, Rashid Mberesero (26) alihuku- miwa kifungo cha maisha jela huku wenzake wawili wakifungwa miaka 41 kila mmoja kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi lililotokea Aprili, 2015 katika chuo hicho na kusababisha vifo vya watu 150.

Mamlaka za Polisi na Jeshi la Magereza nchini Kenya zimethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa Mtanzania huyo alijiua kwa kutumia kipande cha blanketi alilokuwa akitumia katika chumba cha gereza namba 24 Block H.

Polisi nchini humo wamesema mwili wa mfungwa huyo ulikutwa ukining’inia katika vyuma vya dirisha ndani ya chum- ba chake siku ya Jumapili iliyopita huku kipande cha blanketi kikiwa kimefungwa shingoni.

Mkuu wa Ulinzi katika Gereza Kuu la Kamiti, Mark Keitany aliliambia gazeti la People Daily kuwa mfung- wa huyo anahisiwa kujiua saa 9:00 alasiri baada ya wafungwa kumaliza kula chakula chao cha mwisho kwa siku.

“Hatujui ni nini kilicho- sababisha akafanya tukio hilo,” alisema Keitany na kuongeza kuwa wapelelezi wameanza uchunguzi juu ya tukio hilo.

Mberesero alihukumiwa kifungo cha maisha Julai 13, 2019 na alikuwa amekata rufaa juu ya hukumu hiyo na shauri hilo lilikuwa linasubiri kusikilizwa katika Mahakama ya Sheria ya Milimani.

Polisi waliitwa katika eneo la tukio na baadaye kuuchukua mwili kwenda kuuhifadhi kwenye chumba cha kuhifadhi maiti.

Mberesero alihukumiwa pamoja na wenzake wawili, Hassan Edin na Mohamed Abdi, raia wa Kenya waliofungwa kifungo cha miaka 41 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garisa Aprili 2015 na watu 150 kufa.

Watu hao watatu walitiwa hatiani kwa kula njama na kufanya shambulio la kigaidi kwa kushirikiana na kundi la kigaidi la Al- Shabaab.

Shambulio hilo lilikuwa la pili kuua watu wengi Kenya baada ya shambulio lililofanywa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda katika Ubalozi wa Marekani nchini humo mwaka 1998 na kuua watu zaidi ya 200.

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa, upande wa mashtaka ulidai kuwa siku ya shambulio Mberesero alibaki hosteli za chuo hicho na hakuelezea ni kwa nini alikuwa hapo.

Wakati wa shambulio hilo magaidi waliwapiga risasi wanafunzi zaidi ya 200 na kisha kutoroka, am- bako watu 150 waliuawa na takribani 80 kujeruhiwa.

Akizungumza na Habari- LEO jana kuhusu kifo hicho, ofisa mmoja wa ubalozi wa Tanzania nchini Kenya am- baye hakutaka kuandikwa jina lake kwa sababu siyo msemaji wa ubalozi, alieleza kuwa licha ya kusikia juu ya kifo cha Mtanzania huyo gerezani, lakini hawajapewa taarifa rasmi na mamlaka za nchi hiyo.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi