loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ujerumani yatoa euro mil 42.9 kusaidia mtangamano

UJERUMANI imetoa euro milioni 42.9 kusaidia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika programu ya mtangamano wa kikanda na kijamii kama Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja.

EAC na Ujerumani zimekamilisha mazungumzo ya kutolewa kwa fedha hizo zitakazotumika kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Mazungumzo hayo yaliongozwa na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya EAC, Balozi Liberat Mfumukeko na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo katika Shirikisho la Ujerumani (BMZ), Marcus von Essen.

Mazungumzo hayo yalifanyika kwa njia ya mtandao kutokana na mazuio ya kusafiri kwa sababu ya ugonjwa wa covid-19, ambako Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess alishiriki mjini Arusha.

“Tumekuwa tukishiriki kawaida katika nchi za Afrika Mashariki,” alisema Balozi Mfumukeko.

Kwa upande wa Ujeru- mani, von Essen aliipongeza EAC kwa kazi kubwa inayo- fanya kupambana na ugonjwa wa covid-19 katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Von Essen aliipongeza Sekretarieti ya EAC na nchi sita wanachama kwa hatua za mtangamano wa kiuchumi walizofikia ikiwamo Umoja wa Forodha na Itifaki ya Soko la Pamoja.

Alisema Ujerumani itaendela kuwa karibu na EAC na kusaidia mtanga- mano huo, huku akisisitiza ushirikiano zaidi katika miradi ya muda mrefu katika ukanda huo na mtangamano wa kijamii.

Pande zote zilikubaliana kuendelea kukuza ushiriki- ano, ambapo kati ya zaidi ya euro milioni 42.9 zinazohitaji- ka, Ujerumani imehaidi kutoa euro milioni 30.9 kwa ajili ya ushirikiano wa kibiashara na miundombinu ya uchumi.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi