loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dereva wa bodaboda jela maisha kwa kunajisi mtoto

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora imemhukumu dereva wa bodaboda, Benard Mesharck (26) kifungo cha maisha jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumfanyia ukatili wa kijinsia mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Adhabu hiyo ilitole- wa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Jovin Kato kwa kijana huyo aliyekuwa akik- abiliwa na mashitaka la kufanya mapenzi kunyume cha maumbile na mtoto mdogo ambaye jina lake linahifadhiwa.

Akisoma huku ya kesi hiyo, Hakimu Kato alisema kuwa amerid- hika pasipo shaka na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashitaka na kwamba hakuna ad- habu inayositahili zaidi ya kifungo cha maisha. Awali upande wamashitaka ukion- gozwa na wakili Tito Mwakalinga uliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 2, 2020 alipokuwa akimtoa mtoto huyo shule.

Wakili Mwakalinga aliongeza kuwa mshita- kiwa alitenda kinyume na kifungu namba 154 (1)(a) na (2) cha sheria ya makosa ya jinai Sura ya 16 kama ilivyo- fanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Wakili Mwakalinga alidai kuwa mshitakiwa ambaye alikuwa ame- kabidhiwa kumpeleka shule na kumrudisha mlalamikaji siku hiyo baada ya kumtoa shule alimpeleka nyumbani kwake na kisha kum- fanyia ukatili huo huku akijua kwamba ni kosa.

Baada ya mahakama kumtia hatiani upande wa mashitaka uliiomba itolewe adhabu kali kwani kosa alilotenda mshitakiwa ni kinyume na maadili ya Watanzania na pia linaenda kinyume na imani za dini zote hapa nchini ndipo hakimu Kato akamhukumu kifungo cha maisha jela.

JESHI la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Said Shabani ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi