loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampeni za uchaguzi mkuu Uganda zifanyike kwa amani

JANUARI mosi mwaka ujao Uganda itafanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kuchagua Rais atakayeongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Tayari kampeni zimeshaanza kuanzia Novemba 9 mwaka huu na zimepangwa kufikia tamati Januari 12, mwakani.

Inaelezwa kuwa wag- ombea zaidi ya 10 wame- pitishwa kuwania kiti cha urais nchini humo akiwemo Rais aliyepo madarakani Yoweri Museveni, Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine wa chama cha NUP, kamanda wa zamani wa jeshi, Mugisha Muntu na aliyekuwa waziri wa usalama, Jenerali Henry Tumukunde.

Wagombea hao na wen- gine watachuana na Rais Museveni mwenye umri wa miaka 76 ambaye ameion- goza Uganda kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Kampeni hizo za siku 63 zinakabiliwa na changamoto ya kuwapo kwa kanuni za kudhibiti ugonjwa wa Cov- id-19 tofauti na ilivyozoeleka katika kampeni za uchaguzi zilizopita.

Wakati kampeni zikien- delea, tayari kumebainika kuwapo kwa watu walio- fariki kwa vurugu za kisiasa ambao wanadaiwa kufikia 49 kutokana na vurugu zinazo- daiwa kufanywa na wafuasi wa mgombea urais kijana Kyagulanyi ikiwamo ku- fanya maandamano kinyume cha sheria.

Ukiangalia muda wa kampeni tangu zilipoanza na idadi kubwa ya vifo vili- vyokwishatokea, ni dhahiri kuwa wagombea urais na wafuasi wao wanatakiwa kufuata sheria na taratibu za kampeni kwani bila utara- tibu ni vigumu kuendesha kampeni hizo kwa amani na utulivu.

Wagombea na wafuasi wao wanapaswa kuiga nchi jirani za Afrika Mashariki ambazo zimemaliza chaguzi zake kuu hivi karibuni kwa

amani husuani nyakati za kampeni kwa wagombea na wafuasi kufuata sheria na taratibu.

Tanzania na Burundi ni nchi zilizofanya tayaru Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, na zote zimekamilisha kwa amani huku zikiwa huru na kuungwa mkono na waan- galizi wa kitaifa na kimataifa hivyo ni vema wanasiasa wa nchi hiyo kuacha kutumia wananchi kwa maslahi yao ya kukamata dola.

Raia wa Uganda ni vema wakatambue kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi hivyo kampeni zifanyike kwa amani na kufuata sheria kwani vurugu na maandamano hazitasaidia wagombea kufikisha ujumbe wanaotaka.

Ni vema wagombea na vyama vyao kutumia fursa ya kampeni kunadi sera ili wananchi waweze kupiga kura wakijua wanamchagua nani na kwa sababu gani.

Vurugu na kusababisha vifo kwa watu ni doa kwa nchi kwani hakika inaweze- kana wapo waliouawa bila kuwa na hatia au kwa kufuata mkumbo tu.

Katika kampeni hizo poli- si wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia sheria na tara- tibu ili kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 pamoja na kuhakikisha hakuna vurugu zinazotokea.

Kwa yeyote atakayekiuka masharti achukuliwe hatua za kisheria kwani hakuna aliye juu ya sheria na wanan- chi waache kufuata mkumbo kwa kuingia barabarani

na kufanya vurugu bila kuwasilisha hoja za msingi ili ziweze kufanyiwa kazi kwani hakuna linaloshin- dikana kwa mazungumzo iwe wakati wa kampeni au masuala mengine.

Wakati kampeni zikiende- lea, kila la kheri Uganda na tunatarajia uchaguzi kumal- izika kwa amani na usalama kwa manufaa ya nchi hiyo pamoja na ukanda mzima wa Afrika Mashariki (EAC) kwani nchi moja ikiwa na vurugu ni tatizo la ukanda mzima.

TANZANIA imejaliwa na utajiri unatosha kuifanya ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi