loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waliohujumu mali za ushirika wakaliwa kooni

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha na kurudisha mali hizo kwa hiyari kabla ya kuchukuliwa hatua.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya alitoa kauli hiyo jana wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL).

Alisema mali zote za vyama vya ushirika zilizochu- kuliwa bila kufuata utaratibu zitarudi kwenye mikono ya serikali.

Alisema wamefanikiwa kurejesha mikononi mwa serikali mali 59 za ushirika zilizochukuliwa bila kufuata utaratibu ikiwemo viwanja, nyumba, mitambo na vingine vyote vina thamani ya Sh bilioni 68.9 na utaratibu huo ni endelevu.

“Kama kuna mtu ana mali za ushirika kwa njia zisizo sahihi azirudishe kwa hiyari bila hivyo tuna nguvu nyingi za ziada haijalishi zipo wapi lazima tutazipata,”alisema.

Kusaya alisema serikali itakuwa bega kwa bega na benki hiyo ya ushirika ya Kilimanjaro ili kuhakikisha inazaa matunda kwa manufaa ya Watanzania.

“Kama tunaamini katika ushirika lazima tuuheshimu na kulenga kufanya ushirika wa kibiashara katika kum- komboa Mtanzania, tuna- taka kila mwanaushirika awe bilionea,”alisema.

Kwa upande wake, Mwe- nyekiti wa Bodi ya KCBL, Dk Gervas Machimu alisema wameweza kushirikiana na Benki ya CRDB na wana bodi ya pamoja kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.

Alisema serikali ina ndoto ya kuendeleza viwanda katika nchi na kutoa huduma katika kilimo na biashara na uwepo wa benki hiyo utasaidia kue- ndeleza sekta za uzalishaji na kusaidia zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanaotegemea kilimo kunufaika.

Mrajisi wa vyama vya ushirika, Dk Benson Ndiege alisema KCLB ni chama cha ushirika kilichoandikishwa kama benki na kimepata leseni ya kuhudumu kama benki ya ushirika kwa wanan- chi wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga katika kilimo cha kahawa.

Alisema serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kiliman- jaro na Benki ya CRDB wame- fanya kila liwezekanalo ili benki isimame na kuhudumia makundi mbalimbali kama wakulima, wafugaji, wavuvi, wajasiriamali, wafugaji.

“Kama tukiamua leo kui- kuza benki hii kwa kununua hisa tunaweza kuifikisha mba- li, vyama vikuu vya ushirika viko 46 lakini vinavyofanya kazi vizuri viko 30,”alisema.

“Kama tukifanya mabadiliko kwenye sekta ya kilimo, viwanda na uvuvi kama walivyofanya Kenya na kwenye benki ya ushirika wana uwekezaji ndio maana wamefanikiwa na benki yao ni ya tatu kwa ukubwa Kenya,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kilimanjaro Development Forum (KDF), Dk Abubakar Ibrahim alitaka vyama vya ushirika kuchan- gamkia fursa ya uwekezaji kwenye vyama hivyo.

Alisema wanachama wengi wa KDF wamewekeza kwenye benki hiyo. Ofisa Mkuu wa Biashara wa CRDB, Dk Joseph Witts alisema CRDB iliundwa na ushirika na baadaye kuwa benki ya biashara.

“Mikopo yote tunayoitoa kwenye vyama vya ushirika inalipwa vizuri,” alisema.

Alisema wametoa Sh bil- ioni saba kama mtaji kwenye Benki ya KCBL.

Alisema CRDB ina meneji- menti ndani ya benki hiyo na wajumbe wa bodi ya CRDB wengine wako kwenye benki ya KCBL ili kuweza kubore- sha utendaji.

Hivi karibuni serikali ilifanikiwa kurejesha mali za vyama vikuu vya ushirika Nyanza, Geita na Simiyu zenye thamani ya Sh bilioni 61 zilizokuwa zikimilikiwa kinyume cha utaratibu

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa leo amekagua kitalu cha ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi