loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ngorongoro yatinga Afcon U-20

TIMU ya Taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imeweka historia baada ya kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika, Afcon, zitakazofanyika mwakani nchini Mauritania.

Ngorongoro Heroes imepata nafasi hiyo ya kucheza fainali za Afcon 2021 baada ya jana kuifunga Sudan Kusini kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Black Rhino Academy Karatu, Arusha.

Bao hilo pekee lililoipeleka Tanzania katika fainali, lilifungwa na Kassim Haruna katika dakika ya 55, ambapo mbali na kufuzu kwa Afcon 2021, timu hiyo sasa itacheza fainali ya michuano hiyo ya Cecafa kwa wachezaji wenye umri huo.

Tanzania sasa itacheza fainali ya Cecafa dhidi ya Uganda, ambao jana waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika mapema kwenye uwanja huo huo wa Karatu.

Fainali hiyo ya Cecafa itafanyika kwenye Uwanja wa Black Rhino Academy kesho Jumatano, ambapo bingwa atakabidhiwa taji la michuano hiyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Afcon hiyo ya U-20 kushirikisha jumla ya timu 12 badala ya nane kama ilivyokuwa awali, ambapo timu nne za kwanza katika fainali hizo za Afrika, zitafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kwa umri huo nchini Indonesia 2021.

Katika mchezo huo, Ngorogoro Heroes walishambuliana kwa zamu na Sudan Kusini, huku kila upande ukikosa mabao kadhaa baada ya kutokuwa makini walipolifikia lango la wapinzani wao.

Kwa upande wa Uganda, wenyewe wametinga fainali kwa mabao ya Kenneth Ssemakula, beki anayeichezea timu ya Busoga United ya Ligi Kuu ya Uganda katika dakika ya 21.

Dakika nne baadaye, Uganda waliandika bao jingine lililofungwa na Ivan Bogere likiwa ni bao lake la tatu katika mashindano hayo kabla hajafunga bao la pili katika mchezo huo likiwa ni la nne katika mashindano hayo baada ya kufunga kwa penalti.

Kenya walipata bao la kufutia machozi dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika, lililofugwa na Enock Wanyama akimfunga kipa Jack Komakech kwa shuti la karibu.

TIMU ya soka ya Yanga Princess imezidi kujikita kileleni baada ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi