loader
Dstv Habarileo  Mobile
Magufuli apunguzia adhabu wafungwa 256, adai hataki dhambi

Magufuli apunguzia adhabu wafungwa 256, adai hataki dhambi

“WAFUNGWA 256 waliohukumiwa kunyongwa wamepunguziwa adhabu na sasa watafungwa Maisha, Sitaki kutenda dhambi,” amesema Rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza katika uapisho wa Mawaziri 21 na Manaibu 22, Rais Magufuli amesema leo siku ya Uhuru alipaswa anyonge wafungwa 256 lakini ameona kwake ni dhambi kutoa adhabu hiyo.

"Leo siku ya Uhuru, tangu mwaka 2015 nilitakiwa niwe nimeruhusu wafungwa 256 wanyongwe, sijaua hata mmoja na hao 256 nawapunguzia adhabu kutoka kunyongwa sasa watafungwa maisha," amesema JPM na kuongeza kwa kuhoji, " Inawezekana waliohukumiwa  kunyongwa  kwa sababu ya kuua mtu mmoja, mimi naambiwa niue 256 nani atakuwa muuaji mkubwa hapo?.”

Kauli ya Rais Magufuli ni muendelezo wa kauli zake ambazo alishawahi kuzitoa siku za nyuma kuwa hawezi kusaini mfungwa yeyote aliyehukumiwa adhabu hiyo kwenda kunyongwa.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, baada ya mahakama kumtia mtu hatiani na kumsomea adhabu ya kunyongwa mpaka kifo, mamlaka ya kutekelezwa kwa adhabu hiyo inabidi kwanza ipate ridhaa ya Mkuu wa nchi, tena kwa kutia saini.

Mara ya mwisho kwa mfungwa kunyongwa ilikuwa mwaka 1994, enzi za utawala wa Rais wa awamu ya pili  Ally Hassan Mwinyi.

 

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi