Mwandishi wa habari wa kike anayejulikana kwa jina Malala Maiwand, ameuawa kwa kushambuliwa na rasasi alhamisi iliyopita akiwa anaelekea kazini katika Mji wa Jalalabad ulioko Mashariki mwa Afghanistan.
Chanzo cha ripoti hii (BBC) kimesema mpaka sasa hakuna kundi lililotaja kuhusika katika shambulio hilo ambalo pia lilisababisha kifo cha dereva wake.
Maiwand, ambaye ni mwandishi wa habari katika television na Radio Enikass alikuwa akielekea kazini wakati gari lake liliposhambuliwa na watu wasiojulikana
Mauaji hayo yametokea baada ya Nato na EU kutoa tamko la kulaani mauaji yaliyolenga watu mahususi hivi karibuni mjini Afghanistan.