loader
Bocco, Kagere mambo safi

Bocco, Kagere mambo safi

NAHODHA wa Simba, John Bocco na mshambuliaji mwenzake, Meddie Kagere wamesema hawana tofauti yeyote kati yao ila kinachoendelea kwenye mitandao ni watu kutaka kutengeneza habari za uongo.

Bocco na Kagere wametoa ufafanuzi huo kufuatia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuonesha akimkwepa Kagere wakati wanashangilia bao la pili lilofungwa na Clatous Chama kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Bocco  alisema hana tatizo na Kagere na wanashirikiana vyema ila kinachotafsiriwa na watu ni mihemko ya kukosa habari.

“Wanachokitafsiri na wanachokitengeza watu ni mihemuko ya kukosa habari na kutengeneza habari  zisizo na ustaarabu, sina shida na Kagere na wala yeye hana matatizo na mimi,” alisema Bocco.

Naye Kagere aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema hana tatizo na nahodha wake Bocco na hata mchezaji mwingine wa Simba pamoja na timu nzima pia.

“Kwa pamoja tunaungana kumpinga adui anayetaka kutugombanisha kwani sina tatizo na nahodha wala mchezaji mwingine yeyote na timu pia,” aliandika Kagere.

Bocco na Kagere wanacheza nafasi ya ushambuliaji na kwenye mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania walicheza pamoja ingawa hawakufungia timu yao bao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ef7f717acf26cee2a6c402fa6aaaac96.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi