loader
Wabunge wambwaga spika DRC

Wabunge wambwaga spika DRC

SPIKA wa bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),  Jeanine Mabunda ameondolewa katika nafasi yake baada ya wabunge kupiga kura ya maoni kutokana na muswada uliowasilishwa na upande wa upinzani.

Katika kura hiyo iliyopigwa jana, wabunge 281 kati ya wabunge 484 walipiga kura ya ndiyo iliyotosha kumwondoa spika huyo kutoka chama cha Ujenzi wa jamii na Demokrasia (PPRD) cha Rais Mstaafu Joseph Kabila .

Pamoja na chama cha Kabila kuwa na wabunge wengi bado kilishindwa kumlinda spika kutokana na  kuwepo kwa msuguano na mpasuko ndani ya chama.

Kutokana na hali hiyo, kinachotarajiwa nchini DRC ni kuona Waziri Mkuu akijiuzulu. Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kushindwa kwa spika kunasababishwa na kitendo cha Kabila kuchagua spika dhaifu.

Vurugu na ghasia zilitokea ndani ya bunge hilo wiki hii wakati ulipowasilishwa muswada wa kura ya maoni na watu kadhaa walijeruhiwa wakati wanaharakati na wabunge walipoanza kurushiana viti na kuharibu samani ndani ya bunge.

Pamoja na yote hayo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini humo wanasema, huenda isiwe rahisi kwa Rais Tshisekedi kufanya mageuzi ya kiuongozi ikizingatiwa kuwa Joseph Kabila ana ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo.

Mzozo wa hivi karibuni wa kisisia nchini Congo umeibuka tena baada ya rais Félix Tshikedi kutangaza nia yake ya kuvunja bunge .

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c76f11946b5e6470c15521e32d9b1d55.jpg

Papa Francis amesema anatarajia kuzuru Ukraine lakini anasubiri ...

foto
Mwandishi: KINSHASA, DRC

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi