loader
Mfalme wa Morocco afanya mazungumzo na Trump, Abbas

Mfalme wa Morocco afanya mazungumzo na Trump, Abbas

MFALME wa Morocco Mohammed VI amefanya mazungumzo ya simu juzi na Rais wa Marekani, Donald Trump pamoja na Rais wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina Mahmoud Abbas Mazen.

Katika mazungumzo hayo Rais Trump alimjulisha Mfalme Mohammed VI kuwa kutangazwa kwa agizo la rais juu ya uamuzi wa Marekani kutambua kwa mara ya kwanza katika historia yake ardhi yenye mzozo ya Sahara Magharibi kuwa sehemu ya Morroco na kuachana na sera ya muda mrefu ya Marekani juu ya eneo hilo linalodai uhuru kutoka Morocco.

Katika muktadha huo, Marekani imeamua kufungua ubalozi eneo la Dakhla na msingi ukiwa ni masuala ya kiuchumi, kuhamasisha uwekezaji wa Marekani na mchango katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa faida ya wakazi wa maeneo hayo.

Mfalme Mohammed VI kwa niaba ya watu wote wa Morocco alimshukuru Rais wa Marekani kwa hatua hiyo ya kihistoria na pia alitoa shukrani kwa rais huyo wa Marekani kutambua Sahara ya Magharibi kuwa sehemu ya Morocco na kuwa itaimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

Wakati huohuo, Mfalme wa Morocco amesisistiza msimamo wake wa kuunga mkono hoja ya wapalestina kwamba mazungumzo kati ya vyama vya Palestina na Israeli ndio njia pekee ya kufikia suluhisho la mwisho na la mzozo huo wa Mashariki ya Kati.

Katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Al-Quds, chipukizi la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Mfalme Mohammed VI pia hajaacha kamwe kusisitiza juu ya hitaji la kuhifadhi hadhi maalumu ya mji wa Al Quds Asharif na kuheshimu uhuru wa kutekeleza ibada za kidini kwa wafuasi wa dini tatu za imani ya Mungu mmoja na pia sura ya Waislamu ya Al-Quds Asharif na  wa Al-Aqsa.

Katika hatua nyingine,  Jumuiya  ya Kimataifa imeunga mkono uamuzi wa Morocco kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Israel. Maamuzi hayo yanaweka kando misimamo ya miongo mingi ya kuitenga na kutoitambua Israel ambapo sasa mipango ya kufungua balozi kila upande inaendelea.

Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ilisema ni hatua nzuri ambayo inatakiwa ihusishe pande zote zenye mgogoro yaani Israel pamoja na Mamlaka ya Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Arancha Gonzalez Laya alisema nchi yake inaunga mkono hatua hiyo kama sehemu muhimu ya kufikia suluhisho la kudumu katika mzozo wa Mashariki ya Kati lakini haungi mkono kuchukuliwa kwa ardhi ya Saharawi na kupewa Morocco.

Nchi zingine zilizounga mkono makubakliano hayo ni pamoja na Misri, Bahrain, Sudan, Ujerumani na Uingereza.

Upatanishi huo uliofadhiliwa na Marekani unaifanya Morocco kuwa taifa la nne la kiarabu lililoafiki kumaliza uhasama na Israel katika kipindi cha miezi minne iliyopita.

Mataifa mengine ambayo yameanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel ni pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan zilizotangulia kufikia makubaliano na Israel yaliyofanikishwa na Marekani chini ya juhudi za kuitenga Iran na ushawishi wake kwenye kanda ya Mashariki ya kati.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/baed61639ae54c7a2ddb01fd644cc09a.jpg

Papa Francis amesema anatarajia kuzuru Ukraine lakini anasubiri ...

foto
Mwandishi: RABAT, Morocco

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi