loader
Watakiwa kuvaa nepi maalumu kujikinga na Virusi vya Corona

Watakiwa kuvaa nepi maalumu kujikinga na Virusi vya Corona

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga nchini China imewataka wafanyakazi wa ndege zitakazoelekea katika nchi zenye maambukizi ya juu ya Virusi vya Corona kuvaa nepi maalumu ili kujizuia kwenda chooni mara kwa mara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo ilisema matumizi ya milango ya chooni yanaweka afya za wahudumu hao katika hatari ya kuweza kuambukizwa virusi hatari vinavyosababisha ugonjwa wa Covid- 19.

Ushauri huo ni sehemu ya masharti mapya ya namna ya kukabiliana na virusi hivyo kwa wafanyakazi wa ndani ya ndege yaliyotolewa na wataalamu wa afya kutoka mamlaka ya anga ya nchi hiyo.

Masharti hayo yatakuwa yakitekelezwa katika ndege zinazosafiri kuelekea katika vituo vya mataifa yenye viwango vya juu ya tahadhari ya virusi hivyo hatari.

Mashirika mengi ya ndege pamoja na viwanja vya ndege vimekuwa vikiunda na kutekeleza masharti mapya ya namna ya kuepuka maambukizi ya virusi hivyo kwa abiria pamoja na wafanyakazi wa ndani ya ndege.

Katika taarifa yake yenye kurasa 49, Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini China ilieleza utaratibu mpya kuhakikisha kuwa virusi hivyo havisafirishwi kwa ndege kupitia abiria na wafanyakazi wa ndege.

Utaratibu huo utakuwa ukifuatwa kwa ndege zote zinazosafiri kuelekea katika mataifa ambayo kuna maambukizi ya watu 500 kwa kila watu milioni moja. Maagizo haya yanasababishwa na utaratibu wa sasa wa kuvaa barakoa kushindwa kuzuia maambukizi ndani ya ndege.

Miongoni mwa masharti yatakayofuatwa ni pamoja na kuacha siti moja kila baada ya abiria mmoja kama sehemu ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona katika mataifa mbalimbali duniani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5ad9afd1510349876b9594394e5c55e6.jpg

Papa Francis amesema anatarajia kuzuru Ukraine lakini anasubiri ...

foto
Mwandishi: BEIJING, China

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi