loader
Australia yasitisha chanjo iliyoharibu utambuzi wa HIV

Australia yasitisha chanjo iliyoharibu utambuzi wa HIV

SERIKALI ya Australia imesitisha uzalishaji na usambazaji wa chanjo ya Virusi vya Corona baada ya majaribio yake yaliyofanywa kwa wananchi kuanza kuharibu utambuzi wa Virusi vya Ukimwi kwa waathirika.

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison aliwaambia wanahabari kuwa serikali kwa kujali maisha ya kila mwananchi inalazimika kufanya maamuzi yenye athari ya fedha nyingi kwa wazalishaji wa chanjo hiyo.

Chanjo hiyo inayotengenezwa na tawi la uzalishaji wa madawa la Chuo Kikuu cha Queensland (CSL) ilitarajiwa kutolewa katika awamu tatu ili kuwafikia wananchi wote katikia taifa hilo.

 Kwa mujibu wa serikali ya Australia, kingamwili zinazozalishwa kutoka katika chanjo hiyo, mmoja kati ya watumiaji wanne alionesha dalili za uongo za kuwa na Virusi vya Ukimwi wakati hakuwa mwathirika.

Mpaka chanjo hiyo inazuiwa tayari majaribio yalikuwa yamefanyika kwa watu 216 huku majibu yakionesha mafanikio upande wa Virusi vya Sars-Cov-2. Wataalamu wa afya wanasema ili kuliondoa tatizo lililojitokeza itachukua miezi 12 kuweza kulimaliza shida hiyo.

Kutokana na hali hiyo, serikali ya Australia iliamua kuzuia usambazwaji wa chanjo hiyo awamu ya pili nay a tatu ili kuzuia madhara zaidi yanayoweza kusababishwa na chanjo husika.

Profesa kutoka Chuo Kikuu cha Queensland, Paul Young alisema uhitaji wa haraka wa dawa hiyo katika jamii unafanya kupewa kipaumbele cha haraka ili kuendelea kuwakinga wananchi wa taifa hilo na Covid-19.

Taasisi ya uzalishaji chanjo hiyo iliyopo ndani ya Chuo Kikuu cha Queensland ilipewa zabuni ya kutengeneza dozi milioni 51 kwa serikali ya Australia, na kutokana na kuzuiwa serikali itahitaji kiwango cha ziada cha chanjo milioni 20 kutoka Oxford iliyotengenezwa na Kampuni ya Uingereza ya AstraZeneca

Majaribio ya kutoa chanjo kwa wananchi yanatarajiwa kufanyika mpaka mwanzoni mwa Machi 2021 huku chanjo rasmi ikitarajiwa kutanza kutolewa Machi 2021.

Maambukizi ya Virusi vya Corona yamefikia 28,025 nchini Australia huku kiwango cha wananchi waliopona janga hilo kikiwa ni 25,469 na idadi ya wagonjwa waliopoteza maisha imefikia 908.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/36f0e951c182e22a41df7010f2b9674b.jpg

Papa Francis amesema anatarajia kuzuru Ukraine lakini anasubiri ...

foto
Mwandishi: SYDNEY, Australia

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi