loader
Kikwete awasikitikia waendesha bodaboda

Kikwete awasikitikia waendesha bodaboda

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete ameeleza kusikitishwa na ajali zinazosababishwa na waendesha bodaboda zinazopelekea baadhi yao kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu.

Amesema hayo jana katika hafla ya kukabidhi kofia ngumu 850 kwa waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam, kwa ufadhili wa Chama cha Mbio za Magari Tanzania (AAT).

“Takwimu zinasema kwamba, kati ya mwaka 2016 na Juni 2019, watu 2160 wamepoteza maisha kutokana na ajali za bodaboda nchini. Kwa upande wa takwimu za Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa (Muhimbili Orthopedic and Neurosurgical Institute), kati ya Januari 2016 na Desemba 2018, walipokea majeruhi 10,633.  Kati yao waendesha bodaboda 5098, abiria wa bodaboda 3218 na wapiti njia ambao wamepata misukosuko kwa kusukumwa na bodaboda 2319…

“…aidha mwaka 2018 pekee yake, walipokea bodaboda 1813, abiria  1104, na wapitanjia 976,”  alisema Kikwete.

Pamoja na hayo, Kikwete aliwapongeza waendesha bodaboda kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya, ikiwa ni pamoja na kuwarahisishia na kuwasaidia maisha watu wengi.

foto
Mwandishi: Isdory Kitunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi