loader
Arteta afungua  milango kwa Ozil

Arteta afungua milango kwa Ozil

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amefungua milango kwa Mesut Ozil kurejea kwenye kikosi hicho Januari. 

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa nje ya mipango ya kocha huyo Mhispania tangu Machi na hakujumuishwa kwenye kikosi cha Gunners si kwenye michuano ya Ligi Kuu wala ligi ya Europa.

Wakati wote huo amekuwa kwenye kama malumbano na klabu kwenye mitandao ya kijamii huku akifanya uamuzi wa kumlipa mshahara ‘mascot’ wa klabu hiyo aliyefutwa kazi mapema mwaka huu kutokana na janga la covid-19.

Mkataba wa Ozil unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na hatima yake Arsenal inaonekana kama imefika mwisho lakini kwa kauli hiyo ya Arteta pengine huenda kuna nafasi nyingine kwa Mjerumani huyo. 

“Hayupo kwenye kikosi kwa sasa. Naelekeza nguvu zangu kwa wachezaji tulionao. Lakini kwa lolote litakalotokea Januari tuna muda wa kuamua,” alisema Arteta kwenye mkutano na waandishi wa habari juzi.

Kocha wa zamani wa Gunners, Arsene Wenger hivi karibuni alimtetea mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid akisema hakuna ugumu wowote kumuongoza. 

"Sio ngumu kumuongoza ni kijana mwenye kiwango maalum na ni mchezaji mbunifu na anahitaji kufurahi,” bosi huyo wa zamani wa Arsenal aliiambia ESPN.

Wenger alimpa Arteta ushauri jinsi ya kumfanya Ozil kuwa bora.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7b12e1cde69570ed7c3d14a8aec89bf8.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi