loader
Lampard awa  mbogo Chelsea

Lampard awa mbogo Chelsea

KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard amewafyatukia nyota wa timu hiyo akisema wamebetweka baada ya kuanza kwa kishindo Ligi Kuu ya England.

Lampard alisema hayo baada ya kushuhudia timu yake ikipokea kipigo cha pili mfululizo.

Chelsea walilala kwa bao 1-0 dhidi ya Everton mwishoni mwa wiki na Jumanne hii walipokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Wolves huku Pedro Neto akipeleka kilio darajani kwenye dakika za majeruhi.

Chelsea walitangulia kufunga dakika chache baada ya kutoka mapumziko kupitia kwa mshambuliaji Olivier Giroud kabla ya Daniel Podence kuifungia Wolves bao la kusawazisha katikati ya kipindi cha pili.

Wakati Chelsea wakisaka bao la ushindi dakika za mwisho, walijikuta wakiadhibiwa kwa shambulizi la kushtukiza kwa Neto kutumia nafasi hiyo kumpita beki Kurt Zouma na kupiga mpira hafifu uliompita kipa Edouard Mendy.

Lampard ana amini wachezaji wake walipaswa kuendelea kupambana baada ya kuwa wameanza ligi vizuri na kuiweka timu hiyo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

"Kiwango kizuri ndio kinaweza kukupata matokeo na tulikuwa na kiwango kizuri kwa muda mrefu labda pengine wachezaji walidhani tunacheza vizuri na pale mnapodhani kuwa mnacheza vizuri hiki huwa ndio kinatokea."

 

"Labda pengine wachezaji kufikiria kuhusu mechi huku wakiwa wanapumzika. Walifikiri kuhusu usiku wa leo, walifikiri kuhusu Everton. Hii ni Ligi Kuu ya England na kama hauchezi vizuri unapoteza mechi," alisema Lampard.

Lampard pia alilalamikia kitendo cha Chelsea kushindwa kupata matokeo baada ya kutangulia kufunga kipindi cha pili na kuongeza kuwa waliacha mwanya wakati wanasaka mabao zaidi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1642c0d160ed034471f7cb86ef4158fa.jpg

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi