loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ummy aagiza kasi utatuzi kero za Muungano

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu amezitaka wizara ambazo zina hoja 11 za Muungano ambazo hazijapatiwa ufumbuzi, kukaa mara moja ili kuzipatia ufumbuzi wa pamoja.

Ummy aliyasema hayo jana katika kikao cha pamoja baina yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Zanzibar, Dk Khalid Mohammed baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtumba Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.

Alisema wana jukumu kubwa la kuhakikisha Muungano unaimarishwa na kuhakikisha unakuwa imara kwa sababu Muungano huo ndio umoja, usalama na amani ya Tanzania.

“Hatutamvumilia mtu yeyote anayeleta chokochoko na kutaka kuvuruga umoja na mshikamano wa Watanzania,” alisisitiza Ummy.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk Khalid Mohammed alisema serikali zote mbili,  za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), zimefanya kazi kubwa katika kuondoa changamoto kumi ndani ya kipindi cha miaka mitano.

“Kupitia vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ndani ya kipindi cha miaka mitano jumla ya changamoto 21 ziliwasilishwa na kati ya hizo changamoto 10 zimepatiwa ufumbuzi, ni imani yangu kuwa zilizobaki zitapatiwa ufumbuzi kwa kuwa viongozi wetu wana dhamira ya dhati,” alisisitiza Dk Khalid.

Alisema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar imeanza matayarisho ya ujenzi katika kiwanja chenye ukubwa wa ekari 33 katika eneo la Mahoma Makulu, Dodoma ili kurahisha kazi ya uratibu.

“Hakuna sababu ya sisi kubaki Dar es Salaam, tutahakikisha tunahamia Dodoma mapema  iwezekanavyo ili kufanya kazi kwa karibu,”alisema.

Waziri Ummy alimhakikishia Waziri Khalid kufanya kazi kwa pamoja  katika kuimarisha misingi ya amani, umoja na mshikamano kwa maslahi ya pande zote mbili za Muungano.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi