loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa atoa wiki mbili Bandari ya Kagunga kukamilika

Majaliwa atoa wiki mbili Bandari ya Kagunga kukamilika

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameipa wiki mbili Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha Bandari ya Kagunga iliyopo wilayani Kigoma inaanza kutoa huduma.

 Akizungumza mkoani Kigoma wakati wa ziara ya ukaguzi wa bandari hiyo, Majaliwa alichukizwa na namna bandari hiyo ilivyoshindwa kutoa huduma kwa wananchi licha ya ujenzi wake kukamilika mwaka 2017.

 “Tarehe moja mwezi wa kwanza mwakani nataka bandari hii ianze kufanya kazi, muende mkajipange najua hakuna watumishi hapa lakini mnaweza kuwaamisha hata walioko Dar es Salaam waje hapa kutoa  huduma kwa wananchi” amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa ameagiza katika tarehe hiyo soko la kisasa la Kagunga liwe limeanza kufanya kazi ili wananchi wa eneo hilo waweze kufanya biashara.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi