loader
Kaze kumuongezea  nguvu Ntibazonkiza

Kaze kumuongezea nguvu Ntibazonkiza

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema anahitaji kusajili wachezaji wawili kuongeza nguvu katika kikosi chake na suala hilo atalifikisha kwa uongozi.

Kaze ambaye anajivunia usajili wa mchezaji mpya katika kikosi hicho, Saidi Ntibazonkiza amesema anahitaji kupata wachezaji wenye uwezo wa kuongoza wenzao kama Ntibazonkiza na kupiga mipira iliyokufa.

“Nahitaji kupata wachezaji wawili wazoefu kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi hilo nitalifikisha kwa viongozi,” alisema Kaze.

Alisema kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Dodoma Jiji walikuwa wakipata mipira mingi ya kutenga lakini walikuwa wanashindwa kuitumia lakini anashukuru sasa wameanza kuitumia na kufaidika nayo.

Alisema mchezo dhidi ya Dodoma Jiji haukua rahisi baada ya kufungwa dakika za mapema lakini wachezaji wake walipambana na kusawazisha na waliporudi kipindi cha pili walikuwa na lengo la kutafuta ushindi.

Mchezo unaofuata Yanga itacheza na Ihefu mkoani Mbeya.

"Tunajua kuwa Ihefu FC siyo timu rahisi, tunahitaji kujiandaa ili kupata alama tatu lakini tunahitaji sapoti ya mashabiki wetu ili tushinde tuwape furaha," alisema Kaze.

Yanga ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 40 itacheza na Ihefu Desemba 23 badala ya Desemba 26 kama ilivyopangwa awali katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 

 

 

Akizungumza na HabariLEO jana, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema mchezo huo umerudishwa nyuma kutokana na mechi za raundi ya tatu za michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup inayotarajiwa kuchezwa Desemba 25 na 27.

 Katika michuano hiyo Yanga imepangwa kucheza na Singida United na Simba itaivaa Majimaji katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

 

Hafidh alisema wameshaondoka mkoani Arusha kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Ihefu FC.

Naye Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata alisema wanaelekeza nguvu katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro ili waibuke na ushindi.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Yanga, alisema wachezaji wake walipoteza umakini na kuruhusu kufungwa lakini amewapongeza kwa kucheza kwa ushindani.

Kuhusu usajili, alisema kuna marekebisho na ripoti ameipeleka kwa menejimenti hivyo anasubiri watakachoamua.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d764a357648d38f4847f642ce29275b1.jpeg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi