loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Magufuli aomba  Watanzania kuendelea  kumtanguliza Mungu

Rais Magufuli aomba Watanzania kuendelea kumtanguliza Mungu

 

WATANZANIA wameombwa kuendelea kumtanguliza Mungu katika kila jambo wanalolifanya ili aendele kulilinda taifa dhidi ya majanga mbalimbali.

 

Akizungumza katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino jijini Dodoma jana, alipoungana na waumini wa kanisa hilo kusali Misa Takatifu ya Krismasi, ambayo ni maadhimisho ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Rais John Magufuli aliwapongeza pia Watanzania na kuwatakia heri ya Sikukuu ya Krismasi.

 

Baada ya misa hiyo iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo, Padre Paul Mapalala, Rais Magufuli alisema upendo na miujiza ya Mungu kwa Tanzania, inajidhihirisha katika kipindi hiki ambapo dunia inapita katika wakati mgumu wa janga la ugonjwa wa Covid-19 unaosababisshwa na virusi vya corona.

 

“Maelfu ya watu wanaendelea kupoteza maisha kila siku, lakini Tanzania imeepushwa na janga hilo na maisha ya Watanzania yanaendelea kama kawaida,” alisema Rais Magufuli.

 

Aliwaomba Watanzania wote waendelee kumshukuru na kumuomba Mungu, aendelee kulilinda taifa lao dhidi ya ugonjwa huo. Pia aliwataka Watanzania kuwaombea wananchi wa mataifa mengine duniani, waepushwe na corona.

 

Pamoja na kuwatakia heri ya Krismasi, Rais Magufuli aliwataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi za uzalishaji mali, ili kuendelea kujenga taifa pamoja na kuhakikisha wanamtanguliza Mungu kwa kila jambo.

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi