loader
Lampard alalamikia ratiba Ligi Kuu

Lampard alalamikia ratiba Ligi Kuu

FRANK Lampard amesema Chelsea haina faida kwenye mbio za ubingwa kwa vile inalazimika kucheza mara mbili ndani ya saa 48 kwenye Krismasi akiishutumu Ligi Kuu. Chelsea jana ilitarajiwa kucheza na Arsenal jioni kisha itakuwa nyumbani kuisubiri Aston Villa saa 48 baadae.

Manchester City ina ratiba kama hiyo pia, lakini Liverpool na Tottenham Hotspur zitacheza leo na kisha Jumatano huku Manchester United ikitarajiwa kucheza jana na keshokutwa, Lampard anaamini ratiba hiyo haijatenda haki kwa timu yake.

“Ni mechi mbili ndani ya saa 48,” alisema Lampard kwenye mkutano na waandishi wa habari. “Si kwamba najaribu kuwa muuaji hiyo ni pointi muhimu kwetu kwasababu kuna timu nyingine zinawania taji kileleni mwa msimamo zinacheza mechi mbili ndani ya siku tatu.”

“Na nafahamu vizuri kwanini hilo linatokea, mechi itaonyehwa mbashara kama tunavyofahamu ilivyo sasa. Tunacheza na Arsenal kwenye ‘Boxing Day’ (jana) na mechi yetu na Man City sasa imesogezwa Jumapili (Januari 3), kwa hiyo ratiba inaonyesha kwamba hatutacheza na Aston Villa walitaka tucheze Jumanne, walitaka siku ya ziada lakini hatujazingatiwa na wote, Ligi Kuu na watangazaji.”

“Sioni haki iko wapi, nadhani si sahihi na hii sio nzuri kwa wachezaji wanaocheza kwa kiwango cha Ligi Kuu. Msinielee vibaya, Aston Villa wana tatizo kama hilo, hatupati muda wa kupumzika kama wanaopata wenzetu.”

Lampard alisisitiza kitendo cha kucheza mechi ndani ya siku chache kinamaanisha anatakiwa kufanya mzunguko wa kikosi chake wakati Villa itakapokwenda Stamford Bridge

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fdfa10108f923c66152d3c3e7904733f.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi