loader
Dstv Habarileo  Mobile
Askofu Banzi azikwa, skofu Banzi azikwa, Majaliwa ataka aenziwe

Askofu Banzi azikwa, skofu Banzi azikwa, Majaliwa ataka aenziwe

WATANZANIA wameshauriwa kuishi katika umoja, amani na mshi- kamano ili kuendelea kuenzi misingi iliyoachwa na Askofu Anthony Banzi (pichani), aliyefariki dunia Desemba 20 mwaka huu.

Rai hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa ibada ya mazishi ya Askofu Banzi, iliyo- fanyika Kanisa la Mt Anthony wa Padua, Chumbageni jijini Tanga Alisema Askofu Banzi ali- kuwa kiunganisha kizuri baina ya jamii na serikali katika nyanja mbalimbali, hivyo ili kumuenzi hatuna budi kuishi katika misingi aliyotuachia.

“Askofu Banzi alisisitiza kutenda haki miongoni mwa jamii na ni mfano mzuri kwa utumishi wake wa uny- enyekevu na upole, hivyo ni- wasihi tuendelee kumuombea roho yake iishi kwa amani” alisema Majaliwa.

Alisema kuwa serikali imepoteza kiongozi muhimu wa kiroho, ambaye wakati wowote alikuwa tayari kujitoa kwa ajili ya maslahi mapana ya wananchi na taifa lake.

“Tunajivunia mchango wake wa thamani aliotoa katika kudumisha amani na umoja katika kuwapigania Watanzania na hivyo hatuna budi kuyaishi na kuyaenzi ma- tendo yake” alisema Majaliwa.

Aidha, alitoa ushirikiano wake kwa serikali katika nyanja za elimu, afya na maji kwa kuweka miradi mbalim- bali ambayo imesaidia kuleta maendeleo makubwa. Akitoa salamu za Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tan- zania (TEC), Rais wa baraza hilo, Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga alisema Askofu Banzi alikuwa kiunganisha muhimu baina ya madhehebu ya dini zote nchini.

Alisema kuwa hakuna mwanadamu aliyemkamilifu, hivyo aliwataka waumini kote nchini kuendelea kumuom- bea ili roho yake iweze kuwa kwenye amani. “Tuendelee kumuombea marehemu, lakini tusisahau kujiombea na sisi nafsi zetu kama ambavyo maandiko matakatifu yanavyosema ili kutimiza wajibu wa kubwa hapa duniani” alisema Askofu Nyaisonga.

Askofu wa Kanisa An- glikana Dayosisi ya Tanga, Mahimbo Mndolwa alisema marehemu alikuwa kiungani- shi muhimu cha mkoa huo ulipokuwa ukipita kwenye machafuko ya kidini na uhalifu.

“Nakumbuka wakati wa matukio ya uhalifu ya Amboni na mitikisiko ya kidini kule Lushoto, Askofu Banzi ali- weza kutukusanya na kuomba pamoja mpaka pale hali ilipo kuwa shwari, hivyo unaona ni namna gani tumepoteza mtu muhimu mkoani hapa” alisema Askofu Mndolwa.

Akitoa salamu kwa niaba ya wanawake nchini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingi- ra), Ummy Mwalimu alisema marehemu alikuwa mlezi wa wanawake wote nchini, hivyo wanawake wanasikitika wamepoteza baba na mshauri muhimu.

Alisema alikuwa aki- waunganisha wanawake, kwa kauli mbiu yake ya ‘Hekima, Umoja na Amani’ ambayo ilidumisha mshikamano mion- goni mwao.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alisema Askofu Banzi ameaga dunia wakati ambapo Serikali imeanza kutekeleza ndoto yake ya muda mrefu ya kuiwezesha Bandari ya Tanga kufunguka, ili kuinua uchumi wa mkoa huo.

Shigela alisema alipoteu- liwa kuwa mkuu wa mkoa huo, Askofu Banzi alimuomba ashughulikie masuala ya vi- wanda, bandari, reli na uwanja wa ndege. Alisema alimweleza kuwa kama maeneo hayo yatafanya kazi, mkoa huo ungeibua kiuchumi.

foto
Mwandishi: Amina Omari, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi