loader
Kaze: Yanga waliiga Prisons

Kaze: Yanga waliiga Prisons

KOCHA wa Yanga Cedric Kaze alisema kuiga mbinu za wapinzani wao ni sababu iliyowafanya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Bara, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, Rukwa.

Alisema  kwenye mchezo huo wapinzani wao walikuwa wanatumia mbinu ya kupiga mipira mirefu mbele, wachezaji wake waliiga mfumo huo ambao uliwatibulia mipango ya kupata ushindi.

Akitoa tathimini mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kaze alisema malengo yao yalikuwa kwenda kushambulia kupitia pembeni, lakini wachezaji wake walipoteza muelekeo baada ya mbinu yao kushindikana.

“Kipindi cha kwanza tulifuata mchezo wao, malengo yetu yalikuwa ni kushambulia kupitia pembeni ili kupata nafasi ya kwenda kufunga, lakini kitendo cha kuwaacha kutangulia kutufunga walituharibia mbinu, kwani ilitakiwa kupambana kutafuta bao la kusawazisha,”alisema Kaze.

Alisema pamoja na matokeo hayo ya mechi ya ugenini, bado kikosi chake kipo kwenye muelekeo mzuri, kikubwa ni kupigania ubingwa, hivyo wanaenda kujipanga kwa mchezo unaokuja kuhakikisha wanarejesha makali yao.

“Mashabiki wawe na subira kwani wanajua timu inakotoka tunaenda kujipanga kwa mchezo unaokuja kuhakikisha tunafanya vyema,”alisema 

Naye  kocha wa Tanzania Prisons, Salum Mayanga amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kufanikiwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya  Yanga.

Alisema Yanga ni timu  nzuri yenye rekodi nzuri tangu walipoanza ligi, licha ya kwamba wachezaji wake walifanya makosa mengi, lakini walicheza na kutoa upinzani aliotarajia kuuona kwenye mechi hiyo.

Yanga mchezo unaokuja wanatarajia kucheza dhidi ya Mbeya City wakati Tanzania Prisons watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya KMC.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c76ec0ebc71174e81273abfc72f9c631.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi