loader
Warioba na Wasira wahudhuria msiba wa mtoto wa Mwalimu Nyerere

Warioba na Wasira wahudhuria msiba wa mtoto wa Mwalimu Nyerere

Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Steven Wasira wamehudhuria msiba wa mtoto wa Mwalimu Nyerere, Rosemary Nyerere uliopo Msasani Dar es salaam.

Wakizungumza wakati wa kutoa pole nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Msasani, Warioba amesema licha ya Rosemary kuwa na akili, pia aliweza kuishi na watu vizuri.

"Pamoja na kwamba alikuwa mtoto wa rais, Rosemary alikuwa na uwezo wa kuishi na mtu yoyote" amesema Warioba.

Aidha, Mbunge wa Bunda Steven Wasira amesema kuwa familia ya Mwalimu Nyerere imepoteza kiungo muhimu. Familia haijatoa taarifa rasmi ya mazishi

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/625ba4f59f29422d103e18c534c5f53e.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: TAGATO JAMES

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi