loader
Yanga kusajili wawili tu

Yanga kusajili wawili tu

KOCHA wa Yanga Cedric Kaze amesema anahitaji kusajili wachezaji wawili tu ili kukiongezea nguvu kikosi chake kiweze kukabiiana na ushindani wa michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema majina ya wachezaji hao tayari ameshayawasilisha kwenye kamati inayohusika na masuala ya usajili, ambapo mchezaji mmoja ni wa safu ya ushambuliaji, na mwingine ni beki wa kati.

Kaze alitoa kauli hiyo baada ya kikosi chake kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Kaze alisema ushindani alioupata  dhidi ya Tanzania Prisons ni ishara kwamba michezo  iliyosalia itakuwa migumu, hivyo wakifanya maboresho hayo anaamini kikosi chake kitaendelea kuwa tishio.

“Nimeshatoa majina ya wachezaji wawili, mmoja sehemu ya ushambuliaji na mwingine beki wa kati, ambaye ni mzawa, hawa nahitaji kupambana kuwapata kufuta baadhi ya kasoro ambazo naona zitaanza kujitokeza michezo zijazo,”alisema Kaze.

Kaze alisema mshambuliaji ni yule anayesemwa na Injinia Hersi Said ambaye anarekodi bora Afrika, ambaye ligi ya Tanzania Bara hajawahi kutokea na beki wanaamini watapata ingawa itakuwa changamoto.

Kaze alisema licha ya kwamba kikosi chake kipo kwenye muelekeo mzuri wa kubeba taji hilo, wanahitaji kuweka mikakati ya kujipanga kuhakikisha michezo 16 iliyosalia wanashinda kutengeneza uwiano wa pointi na wapinzani wao Simba.

Yanga wanaongoza ligi hiyo kwa pointi 44 walizovuna kwenye michezo 18 na wanatofautiana ya pointi tisa dhidi ya Simba waliopo katika nafasi ya pili lakini wana viporo vya mechi tatu, ambazo kama watashinda vyote, basi watapanda kileleni kwenye msimamo kwa uwingi wa mabao ya kufunga

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e2768cbffa4a229d2dd9c10eea80a873.jpg

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi