loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DK Shein asimikwa kuongoza Chuo Kikuu Mzumbe

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Saba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesimikwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (MU) cha Morogoro.

Dk Shein aliahidi kukiunganisha chguo hicho na vyuo vikuu vingine vya ndani na nje ya nchi ili kuimarisha masuala ya utafiti, taaluma inayoenda na wakati na kutoa ushauri wa kitaaluma.

Dk Shein, alitoa ahadi hiyo jana katika viwanja vya Mahafali ya Chuo kikuu cha Mzumbe baada ya kusimikwa na kukabidhiwa vitendea kazi na aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho na kumaliza muda wake Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta.

Alisema ili chuo hicho kipate hadhi ya kitaifa na kimataifa ni lazima kiwe na uwezo wa kutekeleza majukumu yake makuu ya msingi kwanza kutoa taaluma inayokwenda na wakati ambayo itakayo kiwezesha kuchangia soko la ajira.

Aliahidi atakiunganisha kwenye ushirikiano na chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  ili kuleta mafanikio katika nyanja ya kukuza taaluma na kubadilishana uzoefu ikiwa na lengo la kuongeza soko la ajira hapa nchini hasa kwa vijana.

"Nashukuru Rais Dk John Magufuli kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe hii ni heshima kubwa kwangu na jamii na nimeupokea kwa mikono miwili na ninawaahidi nitafanya kila liwezalo kuuendeleza mafanikio yaliyopatikana kwa muda wote wa uongozi wa mkuu wa Chuo Kikuu Mstaafu Jaji mkuu Mstkatikaafu Samatta"alisema Dk Shein.

Aliahidi kutumia uzoefu wake katika nyanja mbalimbali ikiwemo alipokuwa Mkuu wa Chuo Kikuu SUZA kuiunganisha Mzumbe na chuo hicho kwani ilishawahi kuifanya kwa ukilinganisha na vyuo vikuu vingine duniani katika ushirikiano ili Mzumbe ifikie katika hadhi ya kimataifa.

Alisema pamoja na kuwepo changamoto aliutaka uongozi kuendelea kuwa karibu na jamii katika kutatua matatizo walionayo ambapo alipongeza kwa namna ulivyosaidia kukarabati majengo ya shule ya sekondari Mzumbe.

Makamu Mkuu wa chuo kikuu  hicho, Profesa Lughano Kusiluka,alisema  pamoja  na kuwepo kwa changamoto pamekuwepo na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka 12 ya uongozi wa mkuu wa chuo mstaafu Jaji Mkuu mstaafu Samatta ikiwa pamoja ongezeko la wanafunzi kutoka 5176 mwaka 2009 hadi 11967 mwaka 2020 sawa na asilimia 57.

Profesa Kusiluka, alisema katika kipindi hicho wanataaluma wa shahada ya Uzamivu(PhD) wameongezeka kutoka 45 hadi kufikia 122 sawa na asilimia 85 ambayo ni moja ya mafanikio.

Dk Shein aliteuliwa kuwa mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Novemba 24 mwaka jana na Rais Dk John Magufuli baada ya Jaji Mkuu mstaafu Samatta kumaliza muda wake.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi