loader
RC akaribisha wawekezaji viwanda vya korosho Ruvuma

RC akaribisha wawekezaji viwanda vya korosho Ruvuma

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme ameowaomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi waende kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa za kuongeza thamani ya zao la korosho mkoani humo.

Mndeme alitoa rai hiyo alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo (Tari) Naliendele mkoani Mtwara kujionea kazi za utafiti zinazofanywa ikiwamo za kuongeza thamani kwenye zao la korosho, ufuta, na karanga.

"Nichukue fursa hii kuwaalika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi waje wajenge viwanda ndani ya mkoa wa Ruvuma vya kuongeza thamani kwenye zao la korosho, zao la ufuta na karanga," alisema Mndeme.

Aliseme kazi kubwa ya utafiti imefanywa na kituo cha utafiti cha Naliendele na kwamba ni wakati mwafaka sasa wa wawekezaji kwenda kuwekeza katika mkoa huo.

Alisema mkoa wa Ruvuma una maeneo ya kutosha, malighafi, nguvu kazi, masoko ya uhakika, miundombinu ya barabara na umeme wa uhakika.

"Na mimi niseme kiwanda ambacho kitajengwa uhakika wa soko upo na tunaenda kupanua wigo wa soko na kuongeza mapato kupitia utafiti unaofanyika na pia kuongeza uzalishaji," alisema Mndeme.

Alisema mwekezaji ambaye atakwenda kuwekeza katika mkoa huo hatakutana na urasimu wowote na kwamba ndani ya wiki mbili atapewa ardhi na hati kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda ambacho kitaongeza thamani ya zao la korosho.

Mndeme alisema utafiti umefanywa na unaendelea kufanywa kuongeza thamani pamoja na teknolojia ya kuzalisha bidhaa za kuongeza thamani ili nchi iweze kujenga viwanda ambavyo vitazalisha bidhaa kama vile mvinyo wa korosho, juisi, siagi na maziwa.

Kaimu Mkurungezi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dk Fortunatus Kapinga alisema teknolojia ya kuzalisha bidhaa bora ipo na kwamba kinachohitajika ni viwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa za kuongeza thamani kwenye zao la korosho.

Kapinga alisema kituo hicho ambacho kwa sasa kinazalisha bidhaa ukiwamo mvinyo wa korosho, juisi na siagi na kimetafiti mazao ya kuongeza thamani na namna bora ya kuzalisha bidhaa hizo kupitua technolojia.

Alisema ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya zao la korosho utapanua wigo wa soko, kuongeza uzalishaji na kuongeza ajira kwa wananchi, huku ukimsaidia mkulima kuongeza kipato kutokana na mazao ya zao hilo kuongezwa thamani ambapo awali yalitupwa kama takataka.

foto
Mwandishi: Anne Robi, Mtwara

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi