loader
Trump akubali kuachia madaraka kwa amani

Trump akubali kuachia madaraka kwa amani

RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema yuko tayari kuachilia madaraka kwa amani. Ameyasema hayo siku moja baada ya wafuasi wake kushambulia Bunge la nchi hiyo.

Baada ya akaunti zake za mitandao ya kijamii kurejeshwa jana baada ya saa 12 ikiwamo twitter, Trump alionekana kulaani wafuasi wake walioandamana kuvamia katika Bunge, Capitol Hill, juzi Jumatano.

Wakati Trump wa Chama cha Republican akizungumza hayo, viongozi wa Chama cha Democrats walimtaka kuondolewa ofisini siku 13 kabla ya muda wake kuisha.

Jana katika video yake aliyoeleza anataka makabidhiano ya amani, Trump hakueleza tena kuhusu madai yake ya awali ya wizi wa kura ambayo juzi ndio yaliochochea wafuasi wake kufanya vurugu na kuweka kambi nje ya ikulu yan chi hiyo.

Kauli ya Trump jana ni ya kwanza kukubali hadharani kwamba alishindwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 3 mwaka jana. Mara zote akihutubia au kuzungumza, Trump amekuwa akishutumu uchaguzi huo uliompa ushindi Joe Biden wa Democrats, ulihusisha wizi wa kura.

Katika video yake ya jana, Trump alisema Bunge limeridhia matokeo ya uchaguzi na sasa utawala mpya utaingia madarakani Januari 20, mwaka huu.

“Lengo langu sasa ni kuhakikisha kuwa mchakato wa kukabidhi madaraka unafanyika kwa njia ya amani. Wakati huu tunahitaji maridhiano,” alisema Trump.

Polisi imeshutumiwa kushindwa kudhibiti vurugu hizo zilizoripotiwa kusababisha vifo vya watu wanne. Mkuu wa Polisi amepewa likizo ya lazima baada ya mwanamke kupigwa risasi na kufa ndani ya Bunge la Wawakilishi. Watu kadhaa wanashikiliwa na Polisi kuhusu tukio hilo la uvamizi.

Juzi, kikao cha pamoja cha Baraza ya Seneti na la Wawakilishi kililazimika kusimamishwa kwa muda baada ya wafuasi wa Trump kuingia kwa nguvu ndani ya jingo hilo.

Trump alilaani tukio hilo na kusema watu hao waliyahujumu makao makuu ya demokrasia ya nchini ya Marekani (Capitol Hill) na ameeleza kuwa waliofanya vurugu hizo wanapaswa kulaaniwa na kuadhibiwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1126954436d3dc7f63998056799230f9.jpg

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON DC, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi