loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampuni zinazopima ardhi kuchunguzwa

SERIKALI imeziagiza halmashauri zote kuzichunguza kampuni zinazopima ardhi kabla ya kuzipa kandarasi li kuepuka usumbufu kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula alitoa agizo hilo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro juzi.

"Inasikitisha kuona kampuni zimepewa kandarasi za kupima viwanja vya wananchi kwa ajili ya urasimishaji lakini pamoja na kukusanya fedha za wananchi zimeshindwa kukamilisha kazi hizo huku wakizidi kuteseka," alisema.

Alisem hali hiyo inatokana na kampuni zilizopewa kazi hiyo kutokuwa makini na kwamba kwa kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo kunafifisha jitihada za Rais John Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano za kushirikisha sekta binafsi katika shughuli za kuleta maendeleo.

"Kampuni hizi zimechangisha wananchi wanaotaka kupimiwa viwanja fedha nyingi lakini zimeshindwa kutimiza wajibu wao na sasa baadhi zimepelekwa Takukuru hii ni aibu. Kuanzia sasa hakikisheni mnazipa kandarasi kampuni ambazo zitakuwa na uwezo wa kifedha wa kutekeleza kazi watakazopewa badala ya kuwachangisha wananchi kabla ya kufanya kazi," alisema.

Dk Mabula pia aliziagiza halmashauri zote mkoani Kilimanjaro kufuatilia madeni yote ya kodi za ardhi wanazodaiwa wananchi na taasisi mbalimbali ambayo alisema ni zaidi ya Sh bilioni saba.

"Taarifa zinaonyesha hadi kufikia Desemba, 2020 kulikuwa na wadaiwa sugu ambao walikuwa wanadaiwa zaidi ya Sh bilioni 7 na mlichokusanya hadi kufikia wakati huo ni asilimia 39 tu, hapa hakuna ufanisi wa kikazi", alisema.

Aliziagiza halmashauri hizo kuhakikisha madeni yote yawe yamelipwa kufikia Januari 31, mwaka huu na kwamba kwa wale ambao watakuwa hawajalipa wapelekwe Baraza la Ardhi kwa hatua za ziada kwa mujibu wa sheria.

Aidha, aliziagiza halmashauri zote kutoa ushirikiano unaohitajika kwa maofisa ardhi waliokabidhiwa majukumu ya kufanya kazi katika halmashauri hizo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

"Kuna baadhi ya halmashauri ambazo wamewatenga watumishi wa idara ya ardhi wakati waraka umeweka wazi ya kuwa utumishi wao uko chini ya halmashauri, nitoe wito kwa halmashauri zote watumieni hawa maana majukumu yao yanalenga kufanisha shughuli za halmashauri maana hakuna maendeleo ambayo hayashirikishi raslimali ardhi mahali popote."

"Halmashauri ndiyo wenye mamlaka ya upangaji miji, idara ya ardhi wao kazi yao ni utaalamu utakaofanikisha azma za halmashauri husika hivyo wapeni ushirikiano unaohitajika," alisisitiza.

Dk Mabula ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro alitoa hati za ardhi 22 kwa wananchi na taasisi mbalimbali mkaoni humo, ikiwa ni sehemu ya hati 42 ambazo zimeshakamilika kwa ajili ya  kukabidhiwa wahusika.

ASASI ya UNA Tanzania imeipongeza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Moshi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi